1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Syria na makosa ya mataifa ya magharibi

Sekione Kitojo
15 Machi 2018

Katika  kipindi cha  miaka 7  tangu kuanza  kwa  vita  nchini  Syria mataifa  ya  magharibi  yamefanya  makosa  kadhaa. Iwapo  vita  hivyo vingekuwa  vifupi , hakuna  mtu  anayeweza  kusema  kwa  hakika.

https://p.dw.com/p/2uOYI
Syrien Massenflucht aus Ghuta
Picha: Getty Images/AFP/L. Beshara

Uhakika lakini  ni  kwamba , Mataifa  ya  magharibi  yamepata funzo kutokana  na  makosa  yake.

Vita  vya  Syria  ni  suala  linalohitajika  kujadiliwa  na  wataalamu  wa historia  katika mtaala  maalum wa  historia  ya  mambo  ya  kubuni: Kitu gani  kingetokea  iwapo..... ?  Hususan  swali  hili  linaweza  kuulizwa kwa  kuyatazama  mataifa  ya  magharibi: Vita  hivi vingeendaje , iwapo vingeshughulikiwa  vinginevyo  tofauti na  vilivyoshughulikiwa?  Swali hilo  bila  shaka  halina jibu.Linawahusu watu  kadhaa  ambao wameathirika , ambao  iwapo  mataifa  ya  magharibi  yangelishughulikia vita  hivi tofauti  na  walivyofanya, huenda , wangekuwa  bado wanaishi.

Kwa  mtazamo  wa  sasa  hivi  historia ya  maamuzi  hususan  ya mataifa  ya  magharibi   ni  nafasi  iliyopotea. Baadhi  wamekiri  katika mwaka  2013, walipotambua  kuwa  utawala  wa  rais Bashar al-Assad huenda ulitumia  gesi  ya  sumu  dhidi  ya  wananchi  wake, na  rais  wa Marekani Barack Obama  akatahadharisha  juu  ya  kile  alichokiita "mstari  mwekundu", ambao  katika  hatua  hii ulikwisha  vukwa na kuonya  kwamba  atachukua  hatua. Alipuuzia  kuhusu  sumu  ama  onyo lake,  ama  yote  mawili.

Kwa  hiyo , inaonesha , kulikuwa  na  uwezekano  wa  fursa  ya  mwisho , kuuonesha  utawala  wa  Assad mpaka  wake. Wakati  huo kulikuwa hakuna  nchi zilizokuwa  zinautetea  utawala  huo  kama  Iran  na  Urusi, na  sio  katika  hali  ambayo  nchi  hiyo  inajikuta  hivi  sasa.  Kwa  hivi sasa  katika  kila  eneo  kuna uwiano  wa  nguvu  kubwa  kabisa, kama ilivyo  kwa  Marekani  na  washirika  wake.  Obama  alipoteza uwezekano  huo.

Kersten Knipp, Journalist und Buchautor
Mwandishi wa kujitegemea Kersten KnippPicha: privat

Sababu sahihi kabisa

Wakati  huo  alikuwa  na  sababu nzuri  tu. Kuingilia  kati  kwa  Marekani nchini  Iraq kulitokea  miaka  10 tu  iliyopita, na  kwa  muda  mferu ilikuwa  ni maafa  kisiasa, kimaadili  na  kipropaganda.

Wendawazimu, kwa  misingi  ya  uongo mkubwa  walifanya uvamizi  na kuiweka  Marekani  kuwa  utawala  wenye  kiburi, mabeberu  mamboleo , hali  inayoonesha  kwamba  hadi  leo  hawajaweza  kujitoa.

Ndio sababu  miaka  kumi  baadaye , uvamizi  mwingine  katika mashariki  ya  kati , mara  hii  Syria, ni jambo la hatari.

Kama ingetokea  hadhi  ya Marekani  ingeharibika   zaidi. Pamoja  na kwamba  hali  hiyo  ilikuwa  ngumu lakini hatari  ya  kimkakati , ilikuwa  si sahihi, kuliko hatua  ya  kuingilia  kati ingefanyika. Assad angeacha athari  yoyote ? Iran na  Urusi zingethubutu kupambana  na  uvamizi huo ? Na Obama  angeweza  kuvutia sehemu  ya mataifa  ya  Kiislamu , Washia  pengine  lakini  hata  Wasuni ?

Uvamizi  mwingine ungekuwa  na  maana  ya  mashambulio  mapya  ya wapiganaji  wa  jihadi  nchini  Marekani  ama  hata  barani  Ulaya? Inawezekana  kabisa  kwamba  uvamizi  mwingine  ukaleta matokeo mabaya  zaidi. Hali  ya  sasa  inafahamika  lakini Urusi  na  Iran zimekamata udhibiti  na  kuingilia  kati , hadi mapambano  na  mataifa ya  magharibi  hayawezekani  tena.

Mwandishi: Knipp, Kersten /ZR/ Sekione Kitojo

Mhariri: Daniel Gakuba