1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni : Ni Clinton ama Trump uchaguzi Marekani

Sekione Kitojo
7 Novemba 2016

Kesho Jumanne(09.11.2016) Wamarekani watamchagua rais wao mpya, lakini wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema hakuna mshindi ni kushindwa tu mara hii, wakulaumiwa lakini ni mfumo wa uchaguzi nchini humo.

https://p.dw.com/p/2SGRI
USA Pacific Palisades Stimmabgabe zur US-Präsidentschaftswahl
Picha: picture-alliance/dpa/M. Nelson

Dunia  inasubiri  kwa  hali  ya  wasi  wasi , wakati  Marekani itakapochagua  rais  wake  mpya. Na  bado  inawezekana kwamba  Trump  huenda  akahamia  katika  Ikulu  ya White House  na  mkewe  Melania  na   jamaa  wengine  wa familia  yake  tajiri. Uwezekano  huo  binafsi ni  hali inayoleta wasi  wasi. Kwa nini  linatokea  hili ?  Wamarekani wana  matatizo  gani ?  Inawezekanaje  wakafikiria kuchagua  mtu  ambaye  hana  kabisa  uzoefu  wa  kisiasa katika  kiti  chenye  madaraka  makubwa  kabisa   ya kisiasa   duniani ?

Obama  anaacha  mlima  wa  mambo  ambayo hayajatatuliwa.  Majukumu  ambayo  hayajatatuliwa ambayo  rais Barack Obama  atakuwa  anayaacha  kwa mrithi  wake  ni  makubwa, upande  wa  ndani  ya  nchi  na upande  wa  masuala  ya  kigeni. 

Mageuzi  yake  ya  masuala  ya  afya  bado  hayajakamilika. Syria  ni  mfano  mmojawapo  wa  ombwe  la  madaraka ambalo  linatokea  wakati  polisi  wa  dunia  Marekani wanajiondoa  na  hakuna  mtu  , isipokuwa  Urusi , iko tayari  kuingilia  kati  na  kujaza  ombwe  hilo.

Hususan  wakati  Marekani  ikishindwa  kupata  msaada wa  kijeshi  wa  mataifa  ya  Ulaya   ambapo  Obama amejenga  mkakati  wake  mpya  wa  kujizuwia.

Hatimaye  inawezekana  kwamba  Hillary Clinton  anaweza kushinda  uchaguzi.

Uongozi  wake  katika  maoni  ya  wapiga  kura  unayeyuka , lakini  kwa  bahati  nzuri  kuna  hali  hii  ya  aina  ya kipekee  ya  mfumo  wa  uchaguzi  wa  Marekani , unaotegemea  uhakika  wa  fungu  maalum la kura  katika kila  jimbo kutokana  na  wingi wa wapiga kura wake, maarufu  kama  Electoral  College.

DW Mitarbeiterin Ines Pohl
Mwandishi wa DW Ines Pohl Picha: DW

Lakini  mbali  ya  matokeo , tayari  inaonekana  wazi kwamba  kutakuwa  na  walioshindwa  tu  wakati kinyang'anyiro  hiki  kitakapomalizika.

Katika  miezi  kadhaa  iliyopita  Marekani  imegeuka  kuwa nchi  iliyojengeka  katika  dhana  ya  kula  njama  na  fitina. Hilo linamhusu  zaidi  Donald Trump. Ni  mtu  ambaye hana  wazo  kabisa  kuhusiana  na  masuala  ya  siasa  za kibiashara.  Lakini  ana  uwezo  wa   kuzungumza na kubadilisha  shaka  kuwa  chuki, hofu  ya  kupoteza   kuwa chuki  dhidi  ya  wageni  na  kutokuwa  na  usalama  kuwa hisia  za  kuwa  na  madaraka  makubwa. na  ana  uwezo wa  kujinasibisha  kuwa  ni  mkombozi  pekee  wa  nchi hiyo. Hii  ni  njia  ya  ushindi  ya  fitina.

Kwa sababu  hiyo  watu  wengi  duniani  wanaelekeza kukatishwa  kwao  tamaa  na  wasi  wasi  juu  ya  hali nchini  Marekani  kwa  Donald Trump. Wanamuona  kama mtu  anayehusika  na  kuiweka  Marekani  katika  njia  ya kutoweza  kutawalika.

Lakini  hilo  si  sahihi , takriban katika  dhana  ya  kisiasa. Trump  sie  mwanasiasa , ambaye  kwa  tafsiri anataka kuimarisha  mambo  lakini  anayeweza  kumaumika  iwapo atashindwa  kufanya  hivyo. Trump  ni mfanyabiashara. Kwa  hiyo  lengo  lake  kuu  ni juu  ya  vipi anaweza kubadili  mambo  kwa  faida  yake. Hivi  ndivyo  alivyoweza kuongoza  biashara  yake  ya  kuuza  na  kununua majumba, na  hivi  ndivyo  alivyoshinda uteuzi wa  chama cha  Republican. Na , mtazamo  huu  huenda  ukamfikisha Ikulu  ya  White House.

Mwandishi: Ines Pohl / zr /  Sekione  Kitojo

Mhariri : Yusuf Saumu