1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Mafanikio ya uchaguzi wa Kenya kwenye mabano

5 Machi 2013

Je, tunaweza kusema kuwa uchaguzi wa Kenya umekuwa wa mafanikio katika muktadha wa vifo vya watu 22 pwani mwa nchi hiyo? Hapana, itakuwa ni dhihaka ya hali juu kukubali kwamba ulikuwa kweli wa mafanikio.

https://p.dw.com/p/17qXc

Mashambulizi yaliyofanywa katika jimbo la pwani yalikuwa makubwa na yalisababisha wasiwasi juu ya kutukia kadhia mbaya zaidi. Katika njama zao za kuikwamisha demokrasia kwa manufaa yao ya kibinafsi wale wanaotaka kujitenga katika jiji la Mombasa wamechochea machafuko.

Mkuu wa Idara ya Afrika ya Deutsche Welle, Claus Stäcker.
Mkuu wa Idhaa za Afrika, Claus Stäcker.Picha: DW

Mashambulizi ya Mombasa linakumbusha siyo tu yale yaliyotukia miaka mitano iliyopita nchini Kenya bali yanakumbusha yaliyotukia nchini Afrika ya Kusini miaka 20 iliyopita wakati wa kura ya kihistoria nchini humo.

Pia nchini humo watu waliokuwa na siasa kali za mrengo wa kulia waliokuwa wanataka kujitenga walijaribu kulirudisha nyuma gurudumu la historia. Lakini njama zao hazikufanikiwa. Wapiga kutoka matabaka yote ya jamii walipiga kura na hawakukubali kutetereshwa. Huo ulikuwa wasaa wa kuzaliwa kwa taifa la upinde.

Kwa watu wa Kenya, uchaguzi mkuu huo siyo wa kwanza lakini hauna kifani katika uwazi. Ni uchaguzi uliotayarishwa vizuri sana,bila ya mithili na pia ni uchaguzi uliofuatiliwa kwa makini. Na wapigakura wametoa heshima zao.

Baadhi ya wapiga kura hao walidamka usiku wa manane ili kujipanga katika foleni za kupiga kura. Walisimama katika foleni hizo wakiwa na subira mpaka zamu zao za kupiga kura zilizopofika. Baadhi walinung'unika kutokana na taratibu mpya za kieletroniki kuchelewa.

Walibughudhiwa na taratibu za uchaguzi wa rais, magavana na maseneta ambazo zilikuwaa tata kuliko za hapo awali. Lakini hawakuwatolea watu wengine bughudha hizo.

Baada ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007, Wakenya walirudi nyumbani kwa amani. Hata hivyo palikuwa na wasi wasi juu ya taratibu ambazo hazikuwa wazi, kasoro katika vikaratasi vya kupigia kura na pia kasoro zilizokuwapo katika daftari la wapiga kura.

Lakini wapenda shari walianzisha vurumai mara tu baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.Mgombea mmojawapo, Raila Odinga alitoa malalamiko juu ya wizi wa kura. Lakini safari hii pia watu wengi wana wasiwasi juu ya Kenya.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, alionya kabla ya uchaguzi kwamba Kenya imesimama karibu na ukingo wa kujiangamiza yenyewe. Mashambulizi yaliyotokea Mombasa yameonyesha jinsi mawanda ya usalama yanavyoweza kuwa finyu.

Afrika yaweza kuripuka wakati wowote pia kisiasa

Sasa ni juu ya wadau wakuu kuepusha hali hiyo.Ikiwa wataweka kando maslahi yao ya kibinafsi kwaa manufaa ya taifa, matokeo ya uchaguzi yatailekeza Kenya katika mabadiliko.

Lakini kwa kuwa Uhuru Kenyatta hadi wakati anaongoza kwa mujibu wa taarifa za awali, yaani mwanasiasa anaewakilisha mfumo wa hapo awali - Kenyatta anayekabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu kwenye mahakama ya uhalifuya mjini The Hague; hoja hizo hazionyesha iwapo matokeo ya uchaguzi yataleta mabadiliko. Sheria inapasa kuwa sheria, haudhuri iwapo mgombea amechaguliwa kwa halali au la. Asiyekubali kushindwa si mshindani.

Asiyekubali kushinda siyo mtu ambaye Wakenya wanamhitaji. Matokeo ya uchaguzi ni mwanzo tu. Siku zinazokuja zitaonyesha iwapo kura za Wakenya zina uzito. Mfano ulionyeshwa na Mandela na de Klerk miaka karibu 20 iliyopita. Mfano huo unawezekana pia nchini Kenya.

Mwandishi: Claus Stäcker/DW
Tafsiri: Abdu Mtullya
Mharri: Mohamed Abdul-Rahman