1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Hakuna mabadiliko ya sera kuhusu wakimbizi

24 Aprili 2015

Yalifanyika maombolezo nchini Malta. Viongozi wa taifa na serikali wa mataifa ya Umoja wa Ulaya walikaa kimya kwa dakika moja katika mkutano wao wa dharura mjini Brussels.

https://p.dw.com/p/1FE7v
Sizilien: Ankunft der 27 überlebenden Flüchtlinge der Schiffskatastrophe vor Libyens Küste
Wakimbizi waliokolewa nchini Italia kutoka AfrikaPicha: Reuters

Hii ikiwa ni kuwakumbuka mamia ya wahamiaji , ambao wamefariki siku chache zilizopita katika pwani ya Libya wakijaribu kuingia barani Ulaya. Umoja wa Ulaya unajaribu kutozitwika nchi nyingi za bara la Afrika wajibu wa maafa haya.

Wameahidi kuongeza mchango wao mara tatu zaidi kwa ajili ya shirika la ulinzi wa mipaka nchini Italia na Malta la Frontex na pia kuzisaka meli zitakazokuwa zinasafirisha wahamiaji kinyume na sheria pamoja na kuwaokoa wahamiaji.

Mwandishi wa DW Bernd Riegert anasema katika maoni yake kwamba hakukuwepo na Mabadiliko ya wazi ya sera kuelekea wakimbizi barani Ulaya , licha maafa yaliyotokea.

Umoja wa Ulaya unataka kujitoa kimasomaso.

Kuna maslahi yanayotofautiana sana baina ya wanachama wa Umoja huo. Ni kutokana na mbinyo uliopo ndipo hawawezi kufanya kitu kingine, isipokuwa viongozi hao wa taifa na serikali walilazimika kuuimarisha ujumbe wa sasa wa kulinda mipaka wa Triton.

Hawataki kuonekana hawana utu. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametilia wasi wasi pia hadhi ya msingi ya Umoja wa Ulaya pamoja na haki za binadamu.

Ujerumani, Ubelgiji, Uingereza na wengine zitatuma meli za ziada na wanajeshi, ili takriban kuzuwia maafa mabaya zaidi kutokea tena.

Ujumbe wa "Triton" haupaswi kuonekana kuwa unapanuliwa. Hapa linakuja swali iwapo "Frontex inayofanyakazi kwa pamoja na jeshi la majini la Italia itaweza kuzipata meli zote zitakazokuwa zinasafirisha watu kwa njia haramu. Hapa suala hili haliwahusu watu hawa masikini , ambao licha ya vifo vinavyotokea wanaendelea kupanda maboti hayo, lakini ni kwasababu viongozi wa Ulaya wanataka kuutetea Umoja wa Ulaya.

Fedha zaidi za ulinzi zaahidiwa

Euro milioni tisa kila mwezi mataifa ya Umoja wa Ulaya yanataka kuupatia ujumbe wa Triton. Hii ni kiwango cha gharama ambacho hata ujumbe ambao umemaliza muda wake nchini Italia wa "Mare Nostrum" ulipatiwa.

Kimsingi msimamo wa zamani unatekelezwa hivi sasa , na kwa upande mwingine inaonekana kuwa kuusitisha ule mpango wa Italia wa "Mare Nostrum", ilikuwa ni makosa.

Ukweli hata hivyo ni kwamba "Mare Nostrum" ya Italia haikuondolewa majira ya mapukutiko mwaka jana kutokana na gharama , badala yake ni kwasababu waziri wa mambo ya ndani mhafidhina Angelo Alfaro hakutaka kuwapeleka Italia wahamiaji waliookolewa.

Tatizo hili la msingi hata hivyo halikutatuliwa katika mkutano maalum mjini Brussels. Wakimbizi watapelekwa wapi , wale wanaoomba hifadhi ya kisiasa na wale wahamiaji wa kiuchumi? Suala la kugawanya wakimbizi nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya hazina msimamo wa pamoja.

Kuhusu mabadiliko ya kanuni za Dublin , zinazosema kwamba mkimbizi ,ama anayeomba hifadhi ya kisiasa atahudumiwa katika nchi aliyoingia kwanza, itabidi ifikiriwe upya. Kama ilivyo kwa miaka mingi , mambo hayajabadilika. Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ameweka wazi njia ambayo ni ngumu, ambayo ni kuwagawa wakimbizi miongoni mwa nchi wanachama.

Cameron anataka meli za nchi yake ziwaokoe wakimbizi , lakini bila kumchukua hata mmoja miongoni wa wakimbizi hao, badala yake wawekwe tu nchini Italia.

Umoja wa Ulaya unataka sasa kuthibitisha , iwapo maboti hayo kuyatambua na kupitia ndege za kivita kuyaharibu. Hii inaonekana katika misingi ya kisheria na kiutendaji ni hali ya mkwamo. Kuweka majeshi ya umoja wa Ulaya nchini Libya ambako wakimbizi wanapitia nchini Libya haitarajiwi kabisa.

Mwandishi: Riegert , Bend / ZR/ Sekione Kitojo

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman