1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lazima kukomesha udhalimu

10 Desemba 2015

Katika kuiadhimisha siku hii mwandishi wetu Matthias von Hein anasema haki za binadamu zinahitaji hali ya hewa imara

https://p.dw.com/p/1HL3b
Maandamano ya kupinga adhabu ya kifo nchini Iran
Maandamano ya kupinga adhabu ya kifo nchini IranPicha: picture-alliance/dpa

Katika mwaka huu pia pana sababu ya nguvu ya kusisitiza ulazima wa kukomesha utekelezaji wa kupita kiasi wa adhabu ya kifo, nchini China, Iran au Saudi Arabia.Pia ni wasaa wa kusisitiza juu ya kukomesha mateso, ukatili unaofanywa na polisi na ukandamizaji wa uhuru wa kutoa maoni.

Lakini katika upande mwingine tunaweza kushangilia kutolewa mwaka huu,kwa haki kabisa ,tuzo ya amani ya Nobel kwa jopo la mdahalo wa kitaifa nchini Tunisia.

Katika kuiadhimisha siku ya haki za binadamu leo, pia inahalisi kabisa kutoa mwito kwa viongozi wa wajumbe wanaoshikri kwenye mkutano wa mazingira mjini Paris waache tofauti zao kando na waienzi ibara ya tatu ya tamko la haki za binadamu ili iwe ya zama za leo. Ibara hiyo inalinda haki ya maisha.

Athari za mabadiliko ya tabia nchi zinaua:

Watu wanakufa kutokana na madhara yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Wakati mwingine moja kwa moja. Kwa mfano hali mbaya kabisa za hewa zimeongezeka kwa kiwango kikubwa.

Mwandishi wa maoni Matthias von Hein
Mwandishi wa maoni Matthias von Hein

Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita wati nusu Milioni wamekufa kutokana na mafuriko na dhoruba. Mambo ya hali ya hewa ni ya utata kiasi kwamba haiwezekani kuzibainisha sababu zake kwa uhakika. Lakini hali mbaya za hewa pia zinaua kwa njia nyingne. Kwa mfano kwa kuziyumbisha nchi.

Mfano ni Syria. Vita vya nchini Syria, vilivyosababisha vifo vya maalfu ya watu na kuwafanya mamilioni wengine wayahame makaazi yao, vilitanguliwa na ukame.Wakulima Milioni moja na nusu walilazimika kuyatelekeza mashamba yao na kukimbilia mijini, wakati ambapo Syria ilikuwa tayari inalibeba zigo kubwa la mawimbi ya wakimbizi kutoka Irak. Hata jamii imara ingelitetereka katika mazingira kama hayo.

Mabadiliko ya tabia nchi husababisha mashaka ya usalama: Nchini Syria tatizo liliongezeka kutokana na utawala mbaya na uchochezi kutoka nje

Mfano mwingine ni Boko Haram. Siyo jambo la nasibu kwamba ujio wa Boko Haram unahusiana na kukauka kwa ziwa Chad Ikiwa msingi wa maisha kwa watu Milioni 30,wakulima, mafalahi,wafugaji na wavuvi unanywea na kubakia asilimia 20 tu,mapambano ya kupigania raslimali yanakuwa makali.Na ikiwa umaskini na hali ya kukata tamaa inaenea basi inakuwa rahisi kwa makundi ya magaidi kuwaghilibu vijana.

Kupanda kwa joto kunasababisha mawimbi ya wakimbizi na ya wahamiaji kwa viwango vikubwa. Na upatikanaji wa raslimali, na hasa maji huwa ngondo mara nyingine.

Njaa itaongezeka duniani. Hata tajiri hawataweza kuwalisha watu wote. Katika kila sekunde tatu anakufa njaa mtu mmoja duniani na aghalabu mtoto. Asilani hatuwezi kuikubali hiyo. Jee ni kwa sababu ya mazoea tu au kutokana na kukosekana kwa ubunifu wa kuujenga uchumi wa haki?

Nchi tajiri za viwanda lazima zitangulie mbele kwenye mkutano wa mjini Paris.Wengine wafuate.Unaohusika hapa ni mustakabal wa mwanadamu.

Mwandishi:Matthias von Hein.

Mhariri: Bruce Amani