1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manuel Neuer bado ni chaguo langu la kwanza, asema Flick

23 Aprili 2020

Kocha wa Bayern Munich Hansi Flick amemuunga mkono mlinda lango Manuel Neuer wakati huu ambapo mazungumzo ya kurefusha mkataba wake yanaendelea.

https://p.dw.com/p/3bJx1
DFB-Pokal | FC Schalke 04 vs. FC Bayern München
Picha: Imago-Images/foto2press/M. Ewert

Flick ameliambia gazeti la michezo la Kicker kuwa Neuer atasalia chaguo la kwanza katika nafasi ya mlinda lango. Neuer mwenye umri wa miaka 34 ana mkataba wa kuichezea Bayern Munich hadi mwaka 2021 na inaripotiwa kuwa mazungumzo ya kurefusha mkataba wake yanatajwa kuwa magumu.

Bayern imemsajili kipa Alexander Nuebel kwa uhamisho wa bure akitokea Schalke kuanzia msimu ujao na inakisiwa kuwa kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 atakuwa mpinzani wa Neuer msimu ujao.

Flick pia amemtetea mkurugenzi wa klabu hiyo Hasan Salihamidzic dhidi ya shutuma kufuatia usajili wa Nuebel akisema kuwa ulikuwa ni uamuzi mzuri wa kumsajili kipa huyo aliyemtaja kuwa mlinda lango bora kijana hapa Ujerumani.

Chanzo: