Manila.Kimbunga chauwa watu 15 nchini Philippines. | Habari za Ulimwengu | DW | 31.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Manila.Kimbunga chauwa watu 15 nchini Philippines.

Maafisa nchini Philippines wamesema kimbunga kikali kimelikumba eneo la kaskazini la nchi hiyo na kuuwa kiasi ya watu 15 kutokana na mmomonyoko wa ardhi na mafuriko.

Kimbunga hicho kijulikanacho Cimaron kimepelekea miti kuanguka na kufanya upepo mkali uliokua ukienda kilomita 210 kwa saa.

Watabiri wa hali ya hewa wanawasi wasi kuwa kimbunga hicho kitadumu nchini Philippines siku nzima ya leo.

Jimbo la Isabela lililopo kiaisi ya kilomita 330 kaskazini-mashariki mwa Manila ndilo lililokubwa zaidi na kimbunga hicho ambapo watu watano wamefariki Dunia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com