1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mandeleo Rwanda yapo lakini haki za raia haziheshimiwi

Josephat Nyiro Charo11 Agosti 2010

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameshinda uchaguzi wa rais kama ilivyotarajiwa. Kama tume ya uchaguzi ilivyotangaza jana Jumanne , Kagame amepata asilimia 93 ya kura.

https://p.dw.com/p/OiIH
Rais wa Rwanda, Paul KagamePicha: DW

Kuna upande mwingine wa dikteta huyo anayeleta maendeleo katika nchi hiyo ya kupigiwa mfano katika bara la Afrika. Kabla ya hapo alifanya kampeni iliyogharimu fedha nyingi na kusherehekea mafanikio yaliyopatikana, hususan katika kipindi chake cha miaka saba iliyopita. Hata hivyo, Rwanda ni nchi ya kupigiwa mfano katika bara la Afrika.

Mafanikio ya Wanyarwanda, lakini pia ni mafanikio ya jamii ya nchi fadhili, ambayo imekuwa ikisaidia siasa zake kwa muda wa miaka kadha sasa. Rwanda ni habari nzuri katika habari mbaya za maafa katika bara la Afrika . Inadhihirisha kuwa maendeleo yanawezekana , hata katika bara la Afrika. Nani anataka kuharibu mafanikio haya.

Kabla ya miaka 16 iliopita, kumekuwa na mauaji katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo, wameuwawa watu zaidi ya 800,000 katika mauaji ya kimbari , wengi wao wakiwa Watutsi. Na hii leo, Kigali, mji mkuu wa Rwanda, ni mahali panapotunzwa vizuri, kukiwa na miti na maua mazuri, barabara nzuri, viwanja vilivyokatiwa vizuri majani , katika mji mkuu. Muhimu zaidi ni mfumo mzuri wa shule pamoja na ushauri wa masuala ya shule hata kwa wasichana, mfumo bora unaofanya kazi wa kuwahudumia wagonjwa , kwa kiwango cha bara la Afrika. Na pia sera nzuri na za wazi za uwekezaji. Haya yote ni katika nchi ambamo hali ilikuwa mabaya kama katika nchi nyingine za bara hilo la Afrika. Idadi ya watu inaongezeka kwa kasi, na maeneo ya kilimo kwa ajili ya watu hawa hayatoshi, kuweza kuwapatia chakula. Rwanda haina bandari na haina mali asili.

Mambo mengi yanagharamiwa, hata hivyo. na jamii ya mataifa fadhili. Mataifa haya ya nje yanasaidia kwa kiasi kikubwa mipango ya maendeleo nchini Rwanda yakiwa na hisia mbaya kutokana na kuiacha nchi hiyo pamoja na watu wake wakati wa mauaji. Bila ya misaada hii kutoka nje Rwanda haingeweza kufikia pale ilipo hivi leo na rais Kagame asingekuwa katika hali nzuri.

Malipo haya, hata hivyo, ni gharama kubwa kwa wananchi pamoja na sheria za msingi. Kagame anatawala kwa mkono wa chuma, ambapo wanasiasa wa upinzani wanamwita msaliti, na ndio sababu anawabana. Ukweli ni kwamba , katika wiki zilizopita mwenyekiti wa chama cha kijani aliuwawa kinyama. Mwandishi habari Jean Leonard Rugambage amepigwa risasi muda mfupi baada ya gazeti lake kuandika habari za mauaji yanayofanywa na utawala huo. Mgombea ambaye alikuwa anaoneka kuwa imara Victoire Ingabire yuko katika kizuizi cha nyumbani kwake na hajashtakiwa, ambapo kesi yake imesogezwa mbele, na ndio sababu hakuweza kugombea katika uchaguzi.

Huhitaji mambo mengi katika bara la Afrika kujenga nchi ya chama kimoja. Hii inaonekana dhahiri katika mfano wa Rwanda. Na kuna mtindo mpya unaojitokeza katika bara hilo. Kuna madikteta wanaoleta maendeleo, serikali zinazotekeleza sera za maendeleo lakini zinakanyaga haki za raia. Mtindo huo uko Ethiopia na pia Rwanda.

Mwandishi : Ute Schaeffer / ZR / Sekione Kitojo.

Mhariri : Josephat Charo