1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia wafanya maandamano kuiunga mkono Hamas.

16 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CcDr

Gaza.

Mamia kwa maelfu ya Wapalestina wameingia mitaani mjini Gaza kuonyesha uungaji mkono wao kwa chama cha wanaharakati wa Kiislamu cha Hamas. Maandamano hayo yaliadhimisha miaka 20 ya kuundwa kwa chama cha Hamas. Viongozi katika tukio hilo walitishia kuanzisha vuguvugu jipya la mapambano ya Intifada dhidi ya Israel. Mwezi Juni , Hamas ilichukua udhibiti wa eneo lote la ukanda wa Gaza , na kuyaondoa majeshi ya kundi la Fatah la rais wa Palestina Mahmoud Abbas. Siku ya Ijumaa , Hamas kiliwakamata mshauri mkuu wa serikali ya Abbas ambapo ni utekaji wa kiongozi mkubwa wa aina yake katika miezi ya hivi karibuni.