Malipo ya chini kabisa ya ujira na marufuku ya sigara | Magazetini | DW | 31.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Malipo ya chini kabisa ya ujira na marufuku ya sigara

Mada hizo mbili zilitia leo fora katika safu za wahariri wa magazeti ya Ujerumani.Hasa uamuzi wa Kanzela Angela Merkel kutoungamkono kuweka sheria ya kipimo cha chini cha mishahara ulijadiliwa kwa mapana na marefu.

Gazeti la DIE WELT kuhusu upinzani wa kanzela Markel kuwapo vipimo vya chini kabisa vya mishahara ,lamuungamkono linapoandika:

“Mishahara ya kufa na njaa inapolipwa wafanyikazi na ambayo haiwezi kuhakikisha kuishi,serikali itapaswa hapo kuongeza mapato yao sawa ifanyavyo hii leo chini ya mpango wa Hartz IV.Kwahivyo, serikali inapaswa kuhakikisha mtu anajipatia mapato ya kumhakikishia ataishi uzuri na wala sio kuhakikisha kipimo cha chini ya mshahara….

Isitoshe, vyama vilivyounda serikali ya muungano ya Ujerumani, vinapaswa kuzingatia tena sio juu ya vipimo vya chini vya mshahara katika mapatano kati ya vyama vya wafanyikazi na matajiri wao au chini ya sheria.

Majadiliano ya aina hiyo inamudu tu nchi ambayo haina ukosefu wa kazi,lakini sio Ujerumani yenye zaidi ya watu milioni 4 wasio na kazi wala bazi.”- ni maoni ya DIE WELT.

Gazeti la PFORZHEIMER ZEITUNG linahisi kwamba ikiwa vyama vya wafanyikazi na viwanda haviwezi kuafikiana kuwa na vipimo vya chini maalumu vya mishahara na serikali ina hamu kuona jasho la mfanyikazi linafidiwa inavyostahiki,basi serikali itabidi hapo kutia mkono mfukoni mwake na kugharimia.

Mishahara ya mchanganyiko kutoka mifuko tofauti ni dhamana kwamba wasichana wanaotumika mahotelini na wauzaji katika mabekari ya mikate hawaendelei kulipwa mishahara ya kufa na njaa.

Serikali katika mfumo huu inatia raslimali kuwapatia watu ajira na sio kuendelea katika hali iliopo ya ukosefu wa kazi.Hayo ni matumizi zaidi lakini, yanayozaa matunda-ladai PFORZHEIMER ZEITUNG.

Gazeti la OSTSEEZEITUNG kutoka mjini Rostock limejitokeza na kichwa cha habari:”Kazi njema yafaa kutunzwa”.

Kwa biramu hilo lakumbusha gazeti, Kanzela Angela Merkel alianza wadhifa wake kama waziri mkuu mwishoni mwa mwaka juzi 2005.Kwahivyo, tangu yeye hata chama chake vitapimwa kwa usemi wao huo na hasa juu ya mjadala huu wa malipo ya kuwekwa kipimo cha chini kabisa cha malipo.

Kwani, malipo kama yale ya chini ya euro 2 kwa saa ni aibu kabisa katika nchi tajiri kama Ujerumani.

Na kwavile tawi linalotoa huduma mbali mbali, ndilo linaloathirika na ujira huo mdogo,hoja inayotolewa ya kuzidi kupungua nafasi za kazi pakiwepo kipimo cha chini cha mshahara,haiingii akilini.Kwani marobota hayawezi kutumiwa kama vinyozi kukata watu nywele….lasema OSTSEE ZEITUNg.

Likitugeuzia mada gazeti la ALLGEMEINE ZEITUNG kutoka Mainz lachambua Tume ya UU na vita vyake dhidi ya uvutaji sigara hadharani.Kamishna wa maswali ya afya wa UU Kypriano, anatetea kupigwa marufuku kabisa uvutaji sigara katika nchi zote zanachama wa UU na anazingatia kupitisha sheria kama hiyo.

Gazeti laandika:

Kamishna wa afya wa UU hivi sasa anaegemeza hoja yake ya marufuku uvutaji sigara kwa kushawishi nchi zanacahma ,lakini mtu asihadaike.Kamishna huyo zamani amepanga sheria kutilia nguvu amri hiyo hata ikiwa kwa ssa anapururia kishada chake….

Mwishoe, likitufungia mada hii, gazeti la RHEIN-NECKER-ZEITUNG kutoka Heidelberg laandika:

“Msaidizi bila kutaka bora zaidi kuliko Tume ya UU wasingeipata Lobi ya Ujerumani inayotetea sigara.

Upigaji- marufuku sigara katika mikahawa ya Ujerumani na vilabu vya pombe umeshakata roho tangu miezi kadhaa.Kampeni hii mpya inauzika kabisa kaburini.Kwani,UU ukipitisha sheria yake huko Brussels, ndipo upinzani dhidi ya marufuku hayo, utakaposhika kasi kote nchini…”