1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Malawi yafuta uhusiano wa kibalozi na Taiwan wa miaka 41

15 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CphR

LILONGWE:

Malawi imevunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Taiwan baada ya miaka 41 na vilevile baada ya kuanzisha uhusiano na China.Matumaini ya Taiwan ya kuendeleza uhusiano wake wa kidiplomasia na Malawi ,ulipata pigo pale serikali ya Taipei iliposema kuwa haitaweza kushindana na China ilioahidi kutoa msaada wa dola billioni 6 kwa nchi hiyo ambayo ni maskini kuliko nchi yote ya kusini mwa Afrika.Serikali ya China pamoja na mashirika yake ya Umma,yamewekeza mabillioni ya dola barani Afrika katika juhudi za kupata mali asili za Afrika kwa uchumi wa China ambao unazidi kukomaa na pia kuendelea kuimarika kwa ushawishi wa kisiasa wa Beijing kwa nchi zinazoendelea.