1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makundi ya kuhubiri amani yajitokeza Kenya

Admin.WagnerD20 Februari 2013

Wakati huu zikihesabiwa siku kabla ya uchaguzi wa Machi 4, makundi mbali mbali ya kijamii yamejitokeza kuhubiri amani kuhakikisha uchaguzi huo wa kihistoria unafanyika bila vurugu yoyote.

https://p.dw.com/p/17hqe
Polisi akikabiliana na waandamanajiPicha: AP

Kundi moja la Wakenya mashuhuri linalojiita “Group of Concerned Kenyans Initiative” likiongozwa na Kanali Mstaafu Generali Daniel Opande pamoja na wanachama wengine akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Kenya, Abbas Gullet, limezindua mpango wa kuwashirikisha wanasiasa kuleta amani wakati wa uchaguzi. Sikiliza ripoti ya Alfred Kiti akiwa Nairobi kwa kubonyeza alama ya kusikiliza masikioni hapo nchini.

Mwandishi Alfred Kiti
Mhariri Josephat Charo