1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makoni aungwa mkono na viongozi waandamizi Zimbabwe

1 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DGND

BULAWAYO:

Simba Makoni aliekuwa waziri wa fedha wa Zimbabwe,anaungwa mkono na wanasiasa wawili wa ngazi za juu kutoa changamoto kwa Rais Robert Mugabe katika uchaguzi uliopangwa kufanywa tarehe 29 Machi.Kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Bulawayo,waziri wa ndani wa zamani,Dumiso Dabengwa wa chama tawala cha ZANU-PF na Cyril Ndebele aliekuwa spika wa bunge nchini Zimbabwe,walitamka kuwa wanamuunga mkono Makoni.Dabengwa ni mwanasiasa mwandalizi wa kwanza katika chama tawala kujitokeza hadharani na kumuunga mkono Makoni.

Mgombea urais Makoni amesema,yeye anaungwa mkono na wanachama wengi waliovunjika moyo.Mwanzoni wa mwezi Februari,Makoni aliekuwa mwanachama muhimu katika chama tawala cha Rais Robert Mugabe,ZANU-PF alitangaza kuwa atapambana na Mugabe kugombea wadhifa wa rais katika uchaguzi ujao.Amesema, amevunjwa moyo na utawala wa Mugabe.Rais Mugabe yupo madarakani nchini Zimbabwe tangu nchi hiyo kujinyakulia uhuru wake kutoka Uingereza mwaka 1980.