Majeshi ya nchi za Kiafrika yatakuwa pekee kuweka amani Darfur nchini Sudan
14 Agosti 2007Matangazo
Amesema kumetolewa ahadi za kutosha kutoka nchi za Kiafrika kutaka kuchangia sehemu kubwa sana ya jeshi hilo la mchanganyiko ambalo limekubaliwa na Umoja wa Mataifa wiki iliopita. Alisema mpira sasa uko upande wa Umoja wa Mataifa kutoa kwa haraka fedha zinazohitajiwa kwa ajili ya operesheni hiyo. Umoja wa Mataifa ulipendekeza kuweko jeshi la mchanganyiko kutoka Umoja wa Afrika na Umoja wa Mstaifa kama njia ya kumshawishi Rais wa Sudan, Omar al-Bashir,aruhusu wanajeshi wa kutoka ngambo, ambao yeye alisema hapo mwanzoni kuwa ni sawa na kuukaribisha ukoloni mambo leo.
Othman Miraji alizungumza na Profesa Samuel Mushi wa taaluma za siasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kumuuliza kauli hiyo ya Bwana Konare ina maanisha nini.