1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majeshi ya Israel yaishambulia tena Gaza.

20 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/Dl4j

Gaza:

Majeshi ya Israel yamefanya mashambulio mengine ya anga katika eneo la wapalestina la ukanda wa Gaza leo, baada ya wapiganaji wa Hamas kuyaripua magari mawili yaliokua yakitumiwa kusafirisha misaada ya kiutu hadi Gaza katika kituo cha mpaka na eneo hilo,na kuwajeruhi wanajeshi 13 wa Israel. Jeshi la Israel limesema kiasi ya malori 200 yakiwa na misaada hupitia kituo hicho cha Kerem Shalom kila wiki.Hujuma za kulipiza kisasi za waisraili zimewauwa wapiganaji 6 wakipalestina, wote wakiwa ni wanachama wa Hamas , chama ambacho tokea mwaka jana kinalidhibiti eneo la Gaza na kukataa kabisa kuitambua Israel.