1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majeshi ya Comoro sasa yanadhibiti kisiwa cha Anjouan.

25 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DUF1

Moroni.

Majeshi kutoka katika visiwa vya Comoro vilivyoko katika bahari ya Hindi yanaripotiwa kuwa sasa yanadhibiti kisiwa cha Anzuan baada ya uasi uliodumu kwa muda wa mwaka mmoja.

Maafisa wamesema kuwa majeshi yanayoungwa mkono na jeshi la umoja wa Afrika , yameuteka mji mkuu na uwanja wa ndege bila ya upinzani mkubwa.

Mahali aliko kiongozi wa waasi Mohammed Bakar bado hapafahamiki. Kuchaguliwa kwake kama rais wa kisiwa hicho chenye mamlaka yake ya ndani cha Anzouan mwaka jana kulitangazwa kuwa ni batili na serikali ya visiwa vya Comoro na umoja wa Afrika.

Wakati huo huo habari ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa msemaji wa serikali Abdourahim Said Bakar amesema kuwa kiongozi huyo wa waasi anajaribu kutoroka kwenda kisiwa cha Mayotte kwa boti. Amesema kuwa kanali Mohamed Bakar ameonekana katika kijiji cha Sadanpoini.