1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majadiliano kuleta maelewano kati ya Wakristo na Waislamu

6 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DJi7

VATIKAN:

Baba Mtakatifu Benedikt XVI atakuwa mwenyeji wa mkutano maalum wa viongozi wa Kikatoliki na Kiislamu katika mwezi wa Novemba.Mkutano huo utawaleta pamoja viongozi na wanazuoni wa Kikatoliki na Kiislamu.Uhusiano kati ya dini hizo mbili umekuwa na mvutano tangu mwaka 2006,kufuatia hotuba ya Papa Benedikt iliyohusisha dini ya kiislamu na matumizi ya nguvu.Baadae kiasi ya wataalamu 140 wa Kiislamu walitoa mwito wa kuanazisha majadiliano kwa lengo la kuleta maelewano kati ya dini hizo mbili.

Mkutano wa kwanza utafanywa tarehe 4 hadi 6 mwezi Novemba na utahaudhuriwa na Baba Mtakatifu,makadinali kadhaa na Rais wa Muungano wa wanazuoni wa Kiislamu kutoka Uingereza Sheikh Abdel Hakim Murad.