Maharage yanayochipua sio chanzo cha E.coli | Matukio ya Kisiasa | DW | 07.06.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Maharage yanayochipua sio chanzo cha E.coli

Maafisa wa Ujerumani wamebaini hakuna ushahidi kuwa maharage yanayochipua kutoka kwenye shamba moja kaskazini mwa nchi hiyo ndio chanzo cha mripuko wa bakteria wa E.coli ambao wamesababisha vifo.

default

Bakteria wa E.coli

Wizara ya kilimo katika jimbo la Lower Saxony imeeleza kuwa karibu vipimo dazeni mbili vilivyochukuliwa kwenye shamba lililokuwa likishukiwa vimeonyesha kuwa shamba hilo sio chanzo cha kuripuka bakteria hao.

Uchunguzi katika maharage yanayochipua unaendelea, lakini Reinhard Burger, mkurugenzi wa Taasisi ya Robert Koch amesema uchunguzi wa chanzo cha bakteria hao unaweza usimalizike. Mripuko wa bakteria wa E.coli nchini Ujerumani umewaua kiasi watu 22 na zaidi ya wengine 2,300 barani Ulaya wameambukizwa.

Mawaziri wa kilimo wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana leo kujadiliana kuhusu usalama wa chakula na athari za kiuchumi zilizosababishwa na kitisho hicho, wakati ambapo wanunuzi wana hofu ya kununua mboga mboga kutoka Ulaya.

 • Tarehe 07.06.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/11VV7
 • Tarehe 07.06.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/11VV7

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com