1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mageuzi yahitajiwa kuhusu wakimbizi barani Ulaya

1 Julai 2009

Taratibu zinazotumiwa na Ulaya kuhusiana na wakimbizi zinahitaji kufanyiwa mabadiliko ya kimsingi. Hayo yametamkwa na Amnesty International na Pro Asyl mjini Berlin.

https://p.dw.com/p/Iely
Schwere Zeiten für Flüchtlinge in Italien auf Lampedusa.jpg Illegale Immigranten auf der Insel Lampedusa (Archivbild vom 15.03.2005). Seit fast einem Jahr hat Italien auf Anordnung von Innenminister Giuseppe Pisanu damit begonnen, zahlreiche Immigranten gleich wieder auszufliegen. Nun werden Vorwürfe laut, dass in den Auffanglagern Zustände wie im viel kritisierten US-Hochsicherheitsgefängnis Guantànamo auf Kuba herrschten. Ein Journlist, der sich als vermeindlicher Flüchtling in ein Lager geschmuggelt hatte, berichtet von menschenunwürdigen hygienischen Zuständen und von Schlägen. EPA/FRANCO LANNINO (zu dpa-KORR: "'Wie in Guantànamo' - Schwere Zeiten für Flüchtlinge in Italien" vom 09.10.2005) +++(c) dpa - Bildf
Wakimbizi waliotua kisiwa cha Lampedusa nchini Italia.Picha: picture-alliance/dpa

Mashirika mbali mbali yameamua kuunda jumuiya itakayotetea haki za wakimbizi. Matukio kama vile wakimbizi wa boti wanaozama nje ya mipaka ya nchi za Umoja wa Ulaya;ukiukaji wa sheria za kimataifa unaoshuhudiwa pale wakimbizi wanaposukumizwa baharini na kurejeshwa kule walikotokea au walikopitia; uhaba wa uzoefu wa kushughulikia wakimbizi na pia hali mbaya zinazokutikana katika kambi za wakimbizi ni mambo yaliyochochea kuundwa kwa jumuiya hiyo mpya.Mashirika hayo yanaamini kuwa umma unapaswa kufahamishwa zaidi kuhusu hayo yote.

Mbali na Amnesty International na Pro Asyl, jumuiya hiyo mpya inafungaminisha pia jumuiya za wanasheria na majaji,chama cha Msalaba Mwekundu cha Ujerumani na mashirika mengi mengine yanayohusika na misaada ya kijamii.Kiongozi wa Pro Asyl, Günter Burkhardt alipoeleza zaidi kuhusu jumuiya hiyo mpya alisema kuwa kile wanachotaka ni kuona mageuzi ya kimsingi kuhusu vipaumbele vya sera za Ulaya zinazohusika na wakimbizi na masuala ya uhamiaji.

Kwa maoni ya mashirika hayo, mkondo unaofuatwa na Ulaya haumbatani na haki za binadamu,sheria za kimataifa na hata maamuzi ya Mahakama ya Ulaya kuhusu Haki za Binadamu. Maelfu ya watu wakifariki baharini,mashirika hayo yanataka kufahamishwa waziwazi msimamo wa serikali ya Ujerumani kwani ni dhahiri kuwa suala hilo linahusika na haki za binadamu. Burkardt wa Pro Asyl akaongezea:

"Kile tunachoshuhudia hivi sasa ni mmomonyoko wa msingi unaohusika na jamii yetu, hadhi ya binadamu na uhalali wa haki za binadamu"

Ule mtindo wa kuwakamata wakimbizi katika Bahari ya Mediterenia na kuwarejesha Afrika umekosolewa vikali.Kwani majuma ya hivi karibuni, mamia ya watu walizuiliwa baharini na Italia na wakapelekwa Libya kabla ya kuweza kukanyaga ardhi ya Italia na kuomba ukimbizi. Hatua hiyo imelaniwa na jumuiya hio mpya.Imesema huo ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.Hata Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi duniani UNHCR linataka kuona mageuzi katika utaratibu wa kushughulikia wakimbizi barani Ulaya.Hiyo ni changamoto kubwa kwa Sweden ambayo leo Julai mosi imeshika wadhifa wa urais katika Baraza la Umoja wa Ulaya.

Mwandishi: S.Ripperger/ZR/P.Martin

Mhariri:Abdul-Rahman