Mageuzi ya kidemokrasia yawezekana Uarabuni pia | Matukio ya Kisiasa | DW | 27.01.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mageuzi ya kidemokrasia yawezekana Uarabuni pia

Je,maandamano yalioanzia Tunis na kwenda Cairo,yatafika Sanaa na Damascus pia? Eneo zima la Kiarabu litakumbwa na maandamano na hatimae kujitoa kwenye utawala dhalimu?Kutakuwepo demokrasia badala ya utawala wa mabavu?

Egyptian riot police clash with anti-government activists in Cairo, Egypt, Wednesday, Jan. 26, 2011. Egyptian anti-government activists clashed with police for a second day Wednesday in defiance of an official ban on any protests but beefed up police forces on the streets quickly moved in and used tear gas and beatings to disperse demonstrations. (AP Photo/Ben Curtis)

Polisi wapambana na wapinzani wa serikali mjini Cairo

Jawabu ni la, haitokuwa rahisi hivyo. Kweli sababu zilizozusha maandamano ya kisiasa yanayoenea kutoka nchi moja hadi nyingine, zinafanana na hata azma ni moja. Maandamano hayo yanawalenga watawala wa mabavu na wasomi wanaodhibiti uchumi na siasa. Watawala hao wamestarehe na familia zao ndani ya makasri yao tangu miongo na miongo, huku wakiusahau umma ulio nje. Hawakutambua kuwa wanawajibika kisiasa. Kuwa na maendeleo haimaanishi kunufaisha wachache tu, bali maendeleo hayo yawe kwa wengi. Katika ulimwengu wa Kiarabu, watawala hao hawatambui dhiki za umma zilizo wazi kabisa: Kwa mfano, Je, nitaweza kukidhi mahitaji yangu? Nitapata ajira? Kuna matumaini gani kwa maisha yangu?

Hata hivyo, maandamano ya Tunis hayatokuwa sawa na yale ya wafanyakazi wa gatini mjini Danzig, Poland katika mwaka 1980, na kuleta mapinduzi ya kidemokrasia yatakayoenea katika kanda nzima. Kwani, ulimwengu wa Kiarabu haupo chini ya uongozi mmoja wa kisiasa, kama ilivyokuwa wakati wa Soviet Union ya zamani iliokuwa ikitawala kutoka Moscow. Lakini, wapo wanaoipa jumuiya ya Kiarabu hisia ya umoja. Inahakikishwa kuwa hasira na malalamiko ya umma yanaenezwa. Kwanza kabisa, ni kupitia vyombo vya habari vya Kiarabu. Al Jazeera na Al Arabiya huenda ni vyombo muhimu kabisa katika vuguvugu hilo jipya, kwani picha na habari zinaenezwa kutoka mji mmoja hadi mwingine.

Katika nchi za Kiafrika zenye utawala wa mabavu na zilizo masikini, habari huenda zikazuiliwa, lakini hiyo haiwezekani tena katika ulimwengu wa Kiarabu. Huenda ikawa umma katika nchi za Kiarabu hauna uhuru wa kueleza maoni yao na hawana usemi katika serikali zao, lakini katika mtandao na blogi, raia hao wana usemi muhimu. Hata hivyo, katika nchi nyingi za kanda hiyo, wana blogi na waandishi wa habari wanashinikizwa, kwani serikali zinafahamu kuwa uhuru wa kueleza maoni unaweza kuwaathiri.

Sababu za kijamii zilizozusha maandamano hayo zinaweza kushughulikiwa hapa na pale. Lakini hakuna hakika kama umma wenye hasira na unaotaka mageuzi, utaweza kuridhishwa kwa urahisi hivyo.

Mwandishi: Ute,Schaeffer/ZPR
Mpitiaji: Abdul-Rahman

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com