1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini: Vita nchini Syria, SPD, Macron na wakimbizi

Sekione Kitojo
22 Februari 2018

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo wamejishughulisha  zaidi na hali ya  vita  nchini Syria, wanachama wa chama cha Social Democratic, SPD, kupiga kura kuamua  juu ya  chama chao kujiunga katika serikali ya mseto.

https://p.dw.com/p/2t8Jm
Syrien - Luftangriffe auf Rebellengebiet Ost-Ghuta
Picha: picture-alliance/AP/Syrian Civil Defense White Helmets

Tukianza  na  mada  inayozungumzia  vita  nchini  Syria, gazeti  la Tagesspiegel  la  mjini  Berlin  linazungumzia  kuhusu mkataba  wa Geneva  kuhusu vita:

Mkataba  wa  Geneva unayataka  mataifa  yote duniani kuwalinda raia. Ni marufuku kushambulia  hospitali, kuwazingira  raia  na kuwaweka  katika  hali  ya  kutopata  chakula  kama  silaha  ya kivita ni  marufuku , na  pia ni lazima kulinda misafara ya  mashirika ya  kutoa  misaada. Nchini  Syria  mhariri  anaandika mambo haya tuliyojiwekea  hayana  maana  tena,  hata kwa  suala  la  matumizi ya silaha  za  sumu. Vita  nchini  Syria  imeingia  katika  hali  ya unyama  mkubwa, ni  kutokana  na  kejeli pamoja  na udhaifu wa nchi zenye  dhamana  za  kuwalinda  watu nchini  Syria  kama  Urusi  na Iran. Pia  ni  kutokana  na  Marekani kuonekana  kuchoka. Uturuki pia  ina mchango wake  katika  hili, kwa kujitoa  kutoka  katika maadili  ya  NATO. Na mataifa  mengine  ya  NATO yanatazama  tu.

Mhariri  wa  gazeti  la  Stuttgarter Zeitung  anazungumzia  kuhusu vita ya dunia katika  mfumo  wa  kanda:

Hali  inayosikitisha  nchini  Syria  ni  kwamba  kwa  muda  mrefu sasa  hakuna  tena nchi  yenye  nguvu na  mamlaka, ambayo inaweza  kuzuwia mauaji ya  holela  nchini  humo. Nchini  Syria  hivi sasa  kunatokea  vita ya  dunia  katika  mfumo  wa  kikanda, kila mmoja  anashiriki  katika  mzozo  huo  na  amechukua  jukumu  la kuwa  mpatanishi.

Wanachama wa  SPD

Wanachama  wa  chama  cha  Social Democratic SPD wanapiga kura  kuamua  iwapo  chama  chao kishiriki  katika  serikali ya muungano  na  wahafidhina  wanaoongozwa  na  kansela  Angela Merkel  ama  la. Mhariri  wa  gazeti  la Münchner Merkur anatoa picha  ya  chama  hicho:

Chama  cha  SPD kimo  katika  manung'uniko, na  baadhi  ya vyombo  vya  habari vinaitumia  hali  hiyo. Hata  kama  viongozi  wa juu  wa  chama  hicho , wamefanya  makosa  makubwa ,  inatarajiwa takriban  kuweka  heshima  kidogo pamoja  na haki. Hii ni  kutokana na  haki  ya  wanachama 460,000 , ambao  katika  siku  za  hivi karibuni  sio tu watapiga  kura  kuidhinisha  muungano wa kuunda serikali, lakini  pia  mustakabali  wa  chama  hicho. Wanafanya hivyo  kwa  kujitambua  na hata kama vyama vikuu  vya  Ujerumani vikiwa katika  hali  ya  matatizo.

Kuhusu  sera za rais  wa  Ufaransa kwa wakimbizi, gazeti  la Fuldaer Zeitung  linaandika:

Katika  sera  kuhusu  wakimbizi mahakama  ya  Ulaya iko  wazi, na kwamba  hali  inajirudia  tena. Mapambano  ya  kulinda  mifumo ya utamaduni, dini na siasa,  vitu  ambavyo wakimbizi  kutoka  Afrika kaskazini  wanaonekana  kuwa  wamepitia katika  hali  ya  kutisha sana, wanapaswa  kujishauri iwapo  wanahitajika  kuja  katika  nchi kama  za Ulaya.

Mwandishi: Sekione Kitojo/Inlandspresse

Mhariri: Josephat Charo