1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini Ujerumani

5 Agosti 2009

Meli na wanabaharia wake walioachiliwa huru na maharamia wa Kisomali, kupunguka kwa idadi ya watoto wanaozaliwa nchini Ujerumani ni baadhi ya mada zilizoshughulikiwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo Jumatano.

https://p.dw.com/p/J41D
Ein Hubschrauber fliegt das Handelsschiff "Hansa Stavanger" an, das am Dienstag (04.08.2009) unterwegs zum kenianischen Hafen Mombasa ist. Die somalischen Piraten haben Besatzungsmitglieder der «Hansa Stavanger» offenkundig mit Scheinhinrichtungen terrorisiert. Der 27-jährige Frederik E. aus Brake, 2. Offizier auf dem Schiff, habe seinem Vater berichtet, dass sich Besatzungs-Mitglieder mit verbundenen Augen hinknien mussten und anschließend Gewehrsalven über ihre Köpfe hinweg abgefeuert wurden, berichtete die «Deutsche Schifffahrts-Zeitung» online. Das deutsche Containerschiff mit seinen 24 Crewmitgliedern, darunter fünf Deutsche, wird am Donnerstagabend oder Freitag in der kenianischen Hafenstadt Mombasa erwartet. An Bord ist auch ein Marinearzt. Laut Bundeswehr wird das Schiff von der Fregatte «Brandenburg» begleitet. Foto: Bundeswehr +++(c) dpa - Bildfunk+++
"Hansa Stavanger" ikielekea Mombasa baada ya kuachiliwa na maharamia wa Kisomali.Picha: picture-alliance / dpa

Basi hebu tuanze na gazeti la BILD ZEITUNG linalosema:

"Idadi ya watoto wanaozaliwa Ujerumani inazidi kupunguka. Hakuna nchi nyingine yo yote barani Ulaya ambako huzaliwa watoto wachache zaidi kuliko Ujerumani. Sasa sauti zinapzwa kuhusu msaada wa fedha unaotolewa kwa wazazi. Pesa za walipa kodi zinapotezwa bure! Hivyo kweli kuna mtu alieamini kwamba wanawake kwa ghafla, wataamua kuzaa kwa sababu ya msaada wa fedha kutoka serikalini? Muhimu zaidi ni kuwepo vituo zaidi vya kuwaangalia watoto ili wanawake waweze kuzaa na kufanya kazi bila ya wasiwasi."

Likiendelea, BILD ZEITUNG linauliza: Mbona wanawake katika nchi zingine wanaweza kuwa na watoto na kuendelea kufanya kazi?

"Jawabu ni dhahiri kwani katika nchi hizo wazazi hawapewi pesa mikononi badala yake, pesa hizo huwekezwa katika miradi inayowanufaisha watoto moja kwa moja. Huwepo vituo vya hali ya juu ambako watoto huangaliwa kwa malipo madogo au hata bure. Ujerumani nayo inapaswa kuzingatia hilo."

Na kuhusu ziara ya Bill Clinton nchini Korea ya Kaskazini gazeti la LAUSITZER RUNDSCHAU limeandika hivi:

"Kusema rasmi kuwa Bill Clinton alifanya ziara ya binafsi nchini Korea ya Kaskazini ni jaribio zuri la kutenganisha majadiliano ya kupata uhuru wa wanawake wawili waliozuiliwa nchini humo na yale majadiliano yaliyokwama kuhusu mradi wa nyuklia wa nchi hiyo. Na ziara ya Mmarekani wa ngazi ya juu kama hiyo, imeifurahisha Korea ya Kaskazini inayotaka kuheshimiwa kimataifa-na imeitumia fursa hiyo kuwaachilia huru waandishi wa habari waliokuwa kizuizini. Lakini hiyo haimaanishi kuwa hatua hiyo huenda ikafungua ukurasa mpya katika uhusiano wa nchi hizo mbili."

Na kuhusu meli ya Hansa Stavanger na mabaharia wake walioachiliwa huru na maharamia wa Kisomali, gazeti la NORDWEST ZEITUNG linasema:

"Hasa sasa, baada ya mabaharia wa meli ya Kijerumani "Hansa Stavanger" kuachiliwa huru baada ya kuwalipa maharamia kitita cha pesa,moja limedhihirika: serikali ya Ujerumani kwa dharura inapaswa kuwasilisha mkakati kamilifu juu ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya maharamia wa kisasa. Kuwaachia mateka mikononi mwa maharamia, kwa miezi na miezi, kama ilivyokuwa katika mkasa wa Hansa Stavanger ni hali isiyopaswa kuvumiliwa tena na mateka wala familia zao na ni lazima kwa serikali kuelewa hilo wazi wazi."

Kwa upande mwingine,gazeti la AUGSBURGER ALLGEMEINE likiendelea na mada hiyo hiyo linasema:

"Iwapo siku moja utawala wa kisheria utarejea nchini Somalia na maeneo ya jirani, basi hata katika pwani ya Pembe ya Afrika kutakuwepo hali ya utulivu. Na hilo, ndio liwe lengo la kisiasa. Lakini tutaingojea siku hiyo mpaka lini? Kwani kila wanapolipwa mamilioni, maharamia ndio huzidi kutiwa moyo. Na viongozi wa madola makuu ,huwachilia kikundi cha maharamia kama hao, kuwafanya waonekane kana kwamba ni viongozi wasio na uwezo."

Mwandishi:P.Martin/DPA

Mhariri:M.Abdul-Rahman