1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini Ujerumani hii leo

Kleber, Reinhard23 Januari 2008

Kurejeshwa uhusiano wa kawaida kati ya ujerumani na jamhuri ya umma wa China

https://p.dw.com/p/CwOx
Waziri wa nje wa ujerumani apeana mkono na waziri mwenzake wa ChinaPicha: AP



Mada kuu iliyohanikiza magazetini hii leo ni kuhusu kumalizika enzi baridi katika uhusiano kati ya Ujerumani na Jamhuri ya umma wa China.


Baada ya mvutano wa miezi minne uliosababishwa na ziara ya Dalai Lama katika ofisi ya kansela mjini Berlin,mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi hizi mbili,Steinmeier na Yang wamekubaliana mjini Berlin uhusiano wa nchi zao urejee kua wa kawaida.Kama ishara ya kumalizika mvutano,mawaziri kadhaa  wa serikali pamoja pia na kansela wanatazamiwa kuitembelea China miezi ijayo.Gazeti la WESTFÄLISCHEN NACHRICHTEN la mjini Münster linajiuliza:



"Ndo kusema  hivi sasa kila kitu bam bam?Ugonvi uliosababishwa na Dalai Lama haujaacha dowa katika uhusiano wa pande mbili.Mjini Beijing pia kuna wanasiasa wanaotambua ukweli wa mambo na wenye uwezo wa kuleta wezani kati ya mzozo wa kisiasa na mahitaji ya kiuchumi,hasa katika wakati huu wa shida.Ujerumani inavijunia imani  ya wachina.Busara imeibuka na ushindi mjini Beijing. Kisa cha Dalai Lama kimeshapita-muhimu zaidi ni yajayo.Na huo ndio msingi madhubuti katika uhusiano kati ya Beijing na Berlin.



Gazeti la mjini Berlin Die TAGESZEITUNG nalo pia linajiuliza:



"Eti kweli kila kitu sawa?Sadiki ukipenda.Kwasababu China haikua na shida yoyote na Steinemeier- aliemkataza mjumbe wake anaeshughulikia masuala ya haki za binaadam october iliyopita kukutana na mwanaharakati wa haki za binaadam wa jimbo moja la China,katika ofisi yake mjini Berlin.Ghadhabu za Beijing zilimhusu kansela Angela Merkel mwenye sauti katika siasa ya Ujerumani na China.Ingawa Merkel pia atafika ziarani mjini Beijing october ijayo,lakini ni kwaajili ya mkutano wa kilele kati ya nchi za Umoja wa Ulaya na Asia utakaofanyika mjini humo na kwasababu China isingemudu kutomualika kansela.

Bashasha walizokua nazo Steinmeier na waziri mwenzake Yang Jiechi hazihusu hata chembe kwa hivyo uhusiano kati ya  China na kansela Merkel.Na halitakua jambo la kustaajabisha pia kama wachina watampendelea zaidi mpinzani wake, yaani rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy.China inaonyesha tuu haitaki kuona mambo yanazidi kutokota.