1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini: Mkutano Trump na Putin na EU na Japan na China

Sekione Kitojo
17 Julai 2018

Wahariri wamejishughulisha leo(17.07.2018) na mkutano wa kilele kati ya rais Trump na Putin mjini Helsinki, nchini Finland, mkutano wa kilele baina ya EU na China na mashambulizi ya jeshi la Israel dhidi ya Syria.

https://p.dw.com/p/31a8n
Ergebnisse des Treffen zwischen Putin und Trump

Mhariri  wa  gazeti  la  Hannoversche Allgemeine Zeitung  akiandika kuhusu  mkutano  kati  ya  Donald Trump  na  Vladimir Putin anasema kwamba  ni  vizuri  Marekani  na  Urusi  zinafanya majadiliano  baina  yao, kuliko kwamba  wanafanya  tu mazungumzo. Mhariri anaendelea:

"Hadi  sasa  kuna  habari  nzuri kwamba  mkutano  wao  huo  mjini Helsinki  hatimaye ulifanyika. Undani  wa  mazungumzo  yao  lakini pamoja  na  matokeo  yake  bado yamo  katika  ukungu. Mkutano  wa kilele, ni  mzuri  kama  unavyoonekana, lakini hauondoa mizozo  ya baadaye."

Mjini  Helsinki hakukuwapo  na  maazimio kamili, kulikuwa  na  viongozi wawili  wa  kitaifa  walioshikana  mikono, na  pia  kuhakikisha kwamba  wanaweza  kukutana  tena. Anaandika  hivyo  mhariri  wa gazeti  la Mannheimer Morgen  kuhusu  mkutano  kati  ya  Trump na Putin. Mhariri  anaandika:

"Hii inapendeza katika  hatua  za  mwanzo, katika  kufanya  bora mahusiano  baina  ya  Marekani  na  Urusi. Kwa  mtazamo  wa Ulaya  lakini  huu  ni  mwanzo  wa  ushirikiano  tete, ushirikiano ambao  una  lengo  na  maslahi  ya  binafsi. Ni  mwanzo  wa kukwepa  maadili  yanayowakilisha  Ulaya. Hakuna mtazamo unaoweza kuleta  utulivu."

Mhariri  wa  gazeti  la  Freie Presse  la  mjini  Chemnitz anaandika kuhusu  mkutano  huo  kati  ya  Trump  na  Putin  kwa  kusema, kwamba  kwa  Putin mkutano  huo  ulikuwa kiki  ya  kujitangaza. Mhariri  anaendelea:

"Kwanza mashindano  yaliyokuwa  na  mafanikio  ya  kombe  la  dunia nchini  Urusi,  kisha  mkutano  na  nchi  yenye  nguvu  duniani  katika kiwango  sawa ana  kwa  ana. Hakuna  kitu  bora  kilichowahi kumtokea  Putin  katika  siku hizi  kuliko ilivyokuwa.  Kitu  halisi kilichotokea  katika  mkutano  huo  wa  kilele?  hiyo itakuwa  kazi kwa  ajili  ya uchambuzi  wa  kina."

Mada  nyingine  inahusu  mkutano  wa  kilele wa  kibiashara  kati  ya Umoja  wa  Ulaya, China  na  Japan. Mhariri  wa  gazeti  la  Die Welt la  mjini  Berlin anaandika  kwamba  kutokana  na  wasiwasi  wa kuporomoka kwa haraka kwa  uhusiano kati ya Putin  na  Trump, katika  kivuli  cha  mzozo  wa  kibiashara  duniani kuna  kitu  kipya ghafla  kinamea. Mhariri  anaandika:

"Ushahidi  ni  kwamba  inaelekea  kuna  mabadiliko  ya uhusiano wa mataifa  yenye  nguvu  duniani. Ghafla  China  imeonesha  utayari wa  kufanya  majadiliano  katika  masuala  ya  biashara  na kutangaza kwamba  inataka  kuwekeza  katika  mataifa  ya  Ulaya. Na  pia  Japan  na  mataifa ya  Ulaya  yanajongelea  kwa  kiasi kikubwa. Anataka  Trump  kuhatarisha  pia  TPP  na  Nafta, ukaribioano  baina  ya  Umoja wa Ulaya na  washirika  wake hao wawili  muhimu wa  kibiashara  katika  eneo  la  mashariki  ya  mbali unaonekana."

Mada ya mwisho ni  kuhusu mzozo  katika  mashariki  ya  kati, mhariri  wa  gazeti  la  Suedwest Presse  la  mjini Ulm  anaandika:

"Ndege  za  kivita za Israel zimelishambulia  eneo  la  kaskazini, ikiwa ni jaribio  la  kuondoa uwezekano wa kushambuliwa  upande  wa kusini, ambako  vikosi  vya  jeshi  la  Syria  na  washirika  wake wanakaribia  kwa  kilometa  chache  kabisa  mpaka wake. Kwa Israel  kusongambele kwa  Iran  ama  hata  jaribio  lake, la  kubakia kwa  muda  mrefu  nchini  Syria , ni  sababu  ya  vita. Kuimarika kwa jukumu  la  Iran  katika  nchi  hiyo  jirani  ya  Israel  ni kitisho kwa uhai wa nchi  hiyo."

 

Mwandishi: Sekione Kitojo / Inlandspresse

Mhariri: Josephat Charo