1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko yaua zaidi ya watu 800 nchini Pakistan.

31 Julai 2010

Watabiri wa hali ya hewa wanasema mvua za masika zitaendelea kunyesha kwa siku 10 zijazo.

https://p.dw.com/p/OZ4i
Umoja wa Mataifa umesema kiasi ya watu milioni 1 wamepoteza makaazi yao nchini Pakistan.Picha: AP

Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko mabaya zaidi katika kipindi cha miaka 80 kaskazini magharibi mwa Pakistan, imeongezeka hadi 830. Umoja wa Mataifa umesema kiasi ya watu milioni moja wameathirika na mafuriko hayo. Takriban madaraja 45 yameharibiwa katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa pekee. Madaraja hayo pamoja barabara zilizojaa maji yanavuruga jitihada za waokoaji katika jaribio lao la kuwafikia wahanga. Mito iliyofurika kutokana na mvua za msimu wa masika imefunika vijiji na kusomba miundo mbinu ya mawasiliano.

Überschwemmung in Pakistan
Mafuriko hayo ni mabaya zaidi katika kipindi cha miaka 80 nchini Pakistan.Picha: ap

Umoja wa Mataifa umeahidi kutoa msaada wa kibinadamu kwa wahanga. Serikali ya Ujerumani imetoa Euro nusu milioni kama msaada wa dharura. Marekani inatuma helikopta kadhaa zisaidie katika juhudi za uokozi.

Mwandishi, Peter Moss/Reuters/AFP

Mhariri, Mohamed Dahman