1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwaka mmoja baada ya kusambaratika benki ya Lehman

Abdu Said Mtullya15 Septemba 2009

Jee binadamu amejifunza nini kutokana na mgogoro wa fedha uliosababishwa na kufilisika kwa benki ya Lehman Brothers?

https://p.dw.com/p/Jgtt
Benki ya Lehman Brothers mnamo mwaka 2006.Picha: AP

Mabenki ya Marekani yalisambaratika kama nyumba za udongo katika mvua kubwa, katikati ya mwezi wa desemba mwaka jana.

Jina mashuhuri miongoni mwa mabenki hayo lilikuwa la Lehman Brothers-

Benki hiyo ilifilisika na kusababisha mgogoro mkubwa duniani kote. Jee kilitokea nini na tumepata mafunzo gani?

Kati kati ya mwezi wa septemba mwaka jana mambo yalianzia katika benki ya Merill Lynch. Benki hiyo iliuzwa kwa Bank of Amerika. Ukafuatia muflisi wa benki ya Lehman Brothers. Baadae kampuni ya bima, AIG iliokolewa.

Matukio hayo ndiyo yalikuwa mwanzo wa dunia kutumbukia katika mgogoro mkubwa wa fedha na uchumi.

Wahusika wote walikusanyika ikiwa pamoja na aliekuwa waziri wa fedha wa Marekani wa wakati huo Henry Paulson. Walikutana kwa faragaha. Lakini jambo moja lilikuwa wazi siku ya jumamosi jioni walipokutana.

Merill Lynch iliuzwa kwa Bank of Amerika. Maneja wake Ken Lewis alijaribu kutoa kauli ya kuwaliwaza wadau kana kwamba mambo yalikuwa yanapita tu.Alisema wakati huo kwamba benki yake "inadhamiria kuwa muhudumu bora kuliko wote duniani."

Lakini muda mfupi tu baadae benki ya Lehman Brothers ilitangaza kufilisika baada ya historia ya miaka 158.

Habari zikafuatia kwamba masoko ya hisa dunini kote yalianza kuanguka.

Merrill Lyinch ilikwenda! Hakuna akiefikiria hilo lingeliwezekana. Mabenki ya Lehman na Merrill yalisambaratika kwa mpigo.

Lakini serikali iliiachia Lehman Brothers ianguke wakati benki ya Bear Sterns iliokolewa kiasi cha nusu mwaka tu hapo awali.

Mfumo wa mabenki ulisambaratika duniani kote na kusababisha mgogoro mkubwa wa uchumi. Serikali zililazimika kutenga jumla ya dola trilioni 11 ili kuufufua uchumi wa dunia.

Funzo kubwa linalotokana na mgogoro huo ni kwamba viongozi karibu wote wanakubaliana juu ya ulazima wa kuwepo udhibiti.

Kiini cha matatizo yote hayo kilikuwa uzembe na uroho wa kuchuma fedha ambao haukuwa na mipaka.

Wataalamu bado wanatahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea mgogoro mwingine ikiwa makosa yale yale yatarudiwa.

Mwandishi/Korte J/ZA

Imetafsiriwa / na Mtullya A.

Mhariri/Abdul-Rahman