1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID: Washukiwa wawili wakamatwa

2 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCDF

Polisi nchini Uhispania wamewatia mbaroni watu wawili wanaotuhumiwa kuwa wanachama wa kundi la waasi la ETA la chama cha Basque.

Kukamatwa kwa washukiwa hao kunafuatia ugunduzi wa vifaa vya kuripuka katika uvamizi wa eneo la Basque na eneo jirani la Navarra mwishoni mwa juma.

Polisi wa Basque wako katika hali ya tahadhari kufuatia kukamatwa kwa wanachama wanane wa kundi la ETA wiki iliyopita na kugunduliwa kwa vifaa vya kuripuka na nyenzo za kutengezea mabomu.

Serikali ya Uhispania imesema polisi wanaamini kukamatwa kwa washukiwa hao huenda kukatoa ufumbuzi kwa mashambulio 24 ya kundi la ETA kati ya mwaka wa 2004 na 2006.