1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID: Rais wa zamani wa Argtentina, Isabel Peron atiwa nguvuni Uhispania.

13 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCb4

Polisi wa Uhispania wamesema rais wa zamani wa Argentina, Isabel Peron, ametiwa nguvu nyumbani kwake mjini Madrid.

Jaji wa Argentina ameagiza rais huyo wa zamani akamatwe kutokana na kutoweka mwanaharakati wa mrengo wa kushoto miaka ya sabini.

Bi Isabel Peron pia anachunguzwa na hakimu mwengine wa Argentina kwa uhusiano wake na makundi ya mrengo wa kulia ya wauaji wanaotuhumiwa kuwaua watu takriban elfu moja na mia tano.

Bi Isabel Peron mwenye umri wa miaka sabini na mitano aliingia madarakani mwaka elfu moja, mia tisa na sabini na nne baada ya kifo cha rais wa wakati huo Juan Peron ambaye alikuwa mumewe.

Serikali ya Bi Peron ilipinduliwa mwaka wa elfu moja mia tisa na sabini na sita na amekuwa akiishi uhamishoni nchini Uhispania tangu mwaka elfu moja mia tisa na themanini na moja.