1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID: Iran haitositisha mradi wa nyuklia

1 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBw8

Mpatanishi mkuu wa Iran katika majadiliano yanayohusika na mradi wa nyuklia wa Iran,Ali Larijani na mkuu wa sera za kigeni za Umoja wa Ulaya,Javier Solana wamekamilisha mazungumzo yao mjini Madrid.Majadiliano hayo yanatafuta njia ya kumaliza mgogoro wa nyuklia wa Iran.Viongozi hao wawili wamesema,majadiliano yao yamepata maendeleo na wamekubali kuimarisha mazungumzo hayo kwa kukutana tena uso kwa uso baada ya majuma mawili.Lakini Larijani alisema,Iran haitokubali kuachilia mbali mradi wake wa nyuklia.Hapo awali waziri wa mambo ya nje wa Marekani,Condoleezza Rice alisema,Iran lazima isitishe harakati zake za kurutubisha uranium, ikiwa haitaki kutengwa zaidi na jumuiya ya kimataifa.Marekani na baadhi kubwa ya nchi za Umoja wa Ulaya zina hofu kuwa Iran labda inajaribu kutengeneza silaha za nyuklia.Serikali ya Teheran lakini inashikilia kuwa mradi wake wa nyuklia ni kwa matumizi ya usalama tu.