1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mada tatu tuu zimewashughulisha zaidi wahariri hii leo

Oummilkheir7 Novemba 2007

Mkondo mpya katika uongozi wa chama cha wafanyakazi cha IG Metall na hali katika soko la nishati

https://p.dw.com/p/C7ky

Mkondo mpya katika uongozi wa chama kikuu cha wafanyakazi nchini Ujerumani,hali ya mambo katika soko la nishati na ripoti ya Umoja wa Ulaya kuhusu maendeleo yaliyofikiwa katika juhudi za kuleta mageuzi katika nchi za Balkan na Uturuki,ndizo mada zilizowashughulisha zaidi wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

Tuanze na upepo wa mageuzi katika uongozi wa chama kikuu cha wafanyakazi nchini Ujerumani.Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE limechambua mkutano mkuu wa chama cha wafanyakazi cha IG Metall mjini Leipzig na.”Gazeti kuandika:

“Jurgen Peter amekabidhi kama aimnavyostahiki madaraka aliyokua nayo.Amemuachia nafasi BERTHOLD HUBER,ambae tangu mwaka 2003 alipandishwa daraja kuweza kurithi siku moja wadhifa huo.Ndowa ya busara waliyoifunga wote wawili,ili kunusuru hatima ya chama kikubwa kabisa cha wafanyakazi wa Ujerumani,hata kama imefanikiwa kuliko jinsi wengi walivyofikiria,wakushukuriwa lakini ni Peters aliyeiachia nyota ya Huber ing’are na kuzagaa.Mafanikio yote bayana IG Metall iliyojipatia katika kipindi cha miaka minne iliyopita-motisha katika kupigania haki za wafanyakazi,nyongeza nono za mishahara,kurejesha imani ya wanachama-yote hayo yamepatikana kutokana na juhudi za Huber”-linashadidia Frankfurter Allgemeine.

“Mwanaharakati huyo wa haki za wafanyakazi,Berthold Huber,amechaguliwa kwa wingi mkubwa wa kura-jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa katika historia ya vyama vya wafanyakazi tangu miaka 35 iliyopita.Detlef Wetzel amechaguliwa kua msaidizi wake.Gazeti la Die Welt las mjini Berlin linahisi:

“Uongozi huu mpya unapendelea zaidi ridhaa kwa njia ya mazungumzo na sera za nyongeza ya mishahara zinazoambatana na hali halisi namna ilivyo.Huber na msaidizi wake Detlef Wetzel wanaangaliwa kama mameneja maridadi wanaopigania masilahi ya wafanyakazi na sio kama wakuu wa zamani wa vyama vya wafanyakazi.Hata hivyo kambi mbili za IG Metall hazikutoweka mjini Leipzig.Kila upande unauangalia wa pili kwa jicho la tahadhari.”

Gazeti la NEUE PRESSE la mjini Hannover linahisi :

„Pasitarajiwe mabadiliko makubwa katika sera za uongozi wa IG-METALL.Labda hatua za tahadhari kuweza kusonga mbele-lakini sio za haraka haraka.Muhimu zaidi ni kuhusu msimamo wa kisiasa.Ataweza kweli Huber kukirejeshea uzito wa kisiasa chama hicho cha wafanyakazi?Msimamo wa mtangulizi wake Jürgen Peter wa kuzuwia kila kitu,umefuja hadhi ya IG Metall.

Hali ya mambo katika soko la nishati la Ujerumani imemulikwa na gazeti la Die Welt la mjini Berlin,na kuandika:

„Mtu hawezi hata kidogo kuzungumzia juu ya mashindano ya kibiashara .Kamisheni ya huru ya wataalam iliyoundwa na serikali kuu kuchunguza nini kinahodhiwa na nani,imefichua walakini uliopo:ni mashirika machache tuu yanayotoa huduma za nishati.Zaidi ya hayo mashirika hayo hayo yanashirikiana kana kwamba kuna aina ya kutaka kuyabagua na kuyazuwia mashirika mengine yasihusike na biashara ya nishati.Si jambo la kushangaza kwa hivyo mtu akisikia eti mashirika yamesikilizana juu ya kupanga bei ya nishati.Uvumi wa aina hiyo umeenea na hali ikiendelea hivyo basi serikali kuu italazimika kuingilia kati kuvunja mtindo huu wa mashirika machache kumiliki biashara peke yao-sio tuu kwaajili ya kuwalinda wanunuzi.