1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko Ugiriki

7 Desemba 2008
https://p.dw.com/p/GB1X

Athens:

Mamia ya wafanya fujo wamepambana na polisi katika miji ya Ugiriki ya Athens na Thessaloniki baada ya kijana mmoja wa miaka 16 kupigwa risasi. Mashahidi walisema kijana huyo alipigwa risasi baada ya kundi dogo la vijana kuishambulia gari ya polisi katikati mwa mji mkuu Athens. Saa chache baada ya tukio hilo, polisi ilitoa taarifa ikisema gari iliokua ikipiga doria wakiwemo maafisa wawili wa polisi, ilishambuliwa na kundi la vijana 30 waliokua wakirusha mawe. Televisheni ya Ugiriki iliripoti kwamba kijana aliyepigwa risasi alikimbizwa hospitali, lakini akafariki dunia mara baada ya kuwasili.