1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabibi na mababu hawaruhusiwi kuwatembelea wajukuu Marekani

Oumilkheir Hamidou
30 Juni 2017

Marufuku ya safari yaliyowekwa na rais wa Marekani Donald Trump yanaanza kufanya kazi. Ikulu ya Marekani imetangaza ushindi wa sera mojawapo muhimu ya rais . Hata hivyo huo sio ushindi ambao Trump aliutarajia.

https://p.dw.com/p/2fibp
Stempel visum Symbolbild zu strengen Einreisekontrollen in die USA, picture symbolising strict control for entering the USA
Picha: picture-alliance/blickwinkel/McPHOTO

 

Kile ambacho wakati mmoja kilitajwa kuwa marufuku ya moja kwa moja dhidi ya waislam na kugeuka baadae kuwa marufuku ya muda kwa raia wa mataifa saba yenye wakaazi wengi wa kiislam, kimegeuka hivi sasa kuwa orodha inayotatanisha ya vizuwiizi vya watu kupatiwa viza.

Ahadi alizotoa Trump katika kampeni za uchaguzi, akiahidi kuimarisha usalama kwa kuzuwia watu wanaoingia nchini humo, imebakia kuwa marufuku dhaifu ya usafiri-mpango uliodurusiwa na kuduriwa kwa namna ambayo mtu anaweza kusema hautambulikani.

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Picture alliance/Newscom/O. Douliery/UPI Photo

Kanuni mpya imechujuka na kupoteza uzito

 Mpango huo umepoteza umuhimu wake kufuatia miezi mitano ya kuandamwa mahakamani na kudurusiwa. Awali Trump alilenga kuwapiga marufuku kwa muda watu kutoka baadhi ya nchi, pamoja pia na wakimbizi akiamini  hiyo ni njia mojawapo ya kuwazuwia wale ambao wangeweza kugeuka magaidi katika wakati ambapo serikali yake inaandaa sheria nyengine kali zaidi. Lakini miezi mitano imepita na hakujakuwa na marufuku yoyote-serikali ya Marekani imejitahidi kutunga kesi yenye nguvu kuweza kupata ushindi.

Vizingiti vilivyoanza kufanyakazi tangu alkhamisi usiku na kuruhusiwa kwa muda na mahakama kuu viko mbali kabisa na kanuni aliyotia saini awali rais Trump , kanuni iliyozusha malalamiko, vurugu katika viwanja vya ndege na kuandamwa mahakamani mnamo siku za mwanzo za utawala wake. Amri hiyo ilibatilishwa baada ya kuletwa nyengine ambayo mwenyewe Donald Trump aliitaja kuwa "hafifu" na "sawa kisiasa". Korti kuu ilitaka ifanyiwe marekebisho zaidi" amesema Kari Hong, mtaalam wa sheria za uhamaji kutoka chuo cha sheria cha Boston.

 Amri mpya inaweka masharti ya wakaazi wa mataifa sita yenye wakaazi wengi wa  kiislam  na pia kwa wakimbizi kuomba viza ya kuingia Marekani."Wanatakiwa wawe na uhusiano wa karibu sana wa kifamilia au mafungamano ya karibu sana ya kibiashara.

Maandamano dhidi ya amri ya rais Trump kuwapiga marufuku wakaazi wa nchi sita za kiislam kuingia Marekani
Maandamano dhidi ya amri ya rais Trump kuwapiga marufuku wakaazi wa nchi sita za kiislam kuingia MarekaniPicha: Picture-Alliance/AP Photo/S. Senne

 Iran yalaani kanuni hiyo mpya

Mwongozo kwa ofisi za ubalozi  na ofisi ndogo za ubalozi wa Marekani  unataja mwenye kuomba viza anabidi adhihirishe uhusiano wake, kama mzee, mke, mtoto, wakike au wakiume, mkwe wa kike au wa kiume au mchumba, lakini bibi au babu hawamo katika orodha ya wale wanaotajwa kuwa ni familia.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran  Javad Zarif ameitaja amri hiyo mpya iliyofanyiwa marekebisho kuwa "ni kitambulisho cha aibu cha chuki dhidi ya wairan na ni hatua itakayowazuwia mabibi wa Iran kuonana na wajukuu wao nchini Marekani."

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AP

Mhariri:Yusuf Saumu