1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabalozi wa Iran wawasili nyumbani

Mohammed Khelef3 Desemba 2011

Mabalozi wa Iran waliofukuzwa mjini London, kufuatia mashambulizi dhidi ya ubalozi wa Uingereza mjini Tehran, wamewasili nyumbani asubuhi ya leo (03.12.2011), huku mamia ya watu wakiwapokea kama mashujaa.

https://p.dw.com/p/13Lxh
Kundi la Wairani likiwakaribisha mabalozi wao waliofukuzwa Uingereza.
Kundi la Wairani likiwakaribisha mabalozi wao waliofukuzwa Uingereza.Picha: Mehr

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iran (IRNA), kiasi ya watu 150 walikusanyika katika uwanja wa ndege wa Mehrabad, kuwapokea mabalozi hao wakipiga kelele za kuilaani Uingereza. Hata hivyo, serikali iliwachukuwa na kuwapitisha mlango wa nyuma. Kusitishwa huku kwa shamrashamra za kuwapokea mabalozi, kumechukuliwa kama ni ishara ya mgongano uliopo ndani ya utawala wa Iran.

Serikali ya Uingereza inaamini kuwa, mashambulizi ya Jumanne iliyopita dhidi ya ubalozi wake yalipangwa na serikali, jambo ambalo serikali ya Iran inalikanusha. Hata hivyo, Kiongozi Mkuu, Ayatollah Ali Khamenei, alipongeza mashambulizi hayo na kuionya jumuiya ya kimataifa dhidi ya kushirikiana na Uingereza. Ujerumani, Ufaransa na Uholanzi nazo pia zimewaita nyumbani mabalozi wake. Italia na Hispania zimewaita mabalozi wa Iran nchini mwao kulaani mashambulizi hayo.