1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maaskofu wa DRC waukosoa uchaguzi

Saleh Mwanamilongo13 Januari 2012

Maaskofu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wameukosoa vikali uchaguzi wa rais na bunge uliofanyika Novemba mwaka jana, wakiuita kuwa ni aibu kwa taifa hilo na kwamba kasoro zilizotokea zimeyaathiri matokeo yake.

https://p.dw.com/p/13j0T
Etienne Tshisekedi (kushoto) na Rais Joseph Kabila.
Etienne Tshisekedi (kushoto) na Rais Joseph Kabila.Picha: picture alliance/dpa/DW-Fotomontage

Iki ni zaidi ya mwezi tangu matokeo ya uraisi kutangazwa na mengine ya ubunge yakiendelea kupatikana kidogo kidogo, maaskofu hao wameiomba Tume ya Uchaguzi (CENI) kurekebisha makosa mengi yaliyofanyika au vyenginevyo Tume hiyo ijiuzulu.

Maaskofu hao pia Wamelaani umwagikaji wa damu, lakini wametaka kufanyike mazungumzo baina ya wanasiasa ili kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Hayo yanaytokea wakati waumini wa Kikristo katika mji mkuu Kinshasa wakipanga maandamano mwezi ujao kwa dhamira ya kuomba "ukweli wa uchaguzi".

Kanisa nchini DRC lina nguvu kiasi fulani kwa wafuasi wake, ingawa si kila mara nguvu hizo hutumika kuathiri mchakato wa mageuzi.

Ripoti: Saleh Mwanamilongo
Mhariri: Othman Miraji