1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano makubwa mjini Rangun

23 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNH

Rangun:

Maandamano makubwa kuwahi kuandaliwa tangu wimbi la malalamiko mwezi uliopita,yanafanyika dhidi ya utawala wa kijeshi nchini Birma.Kwa mujibu wa ripoti za waandishi habari,watu kati ya elfu kumi hadi elfu 20 wanaandamana katika mji mkuu Rangun.Maandamano hayo yanaongozwa na maelfu ya watawa wa kibudha.Vikosi vya usalama havikuingilia kati –ripoti hizo zinasema.Maandamano hayo yalianza Agosti iliyopita kupinga kupandishwa bei ya mafuta ya petroli na gesi.