1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano dhidi ya vita vya Irak

18 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHq

Maelfu ya waandamanaji wameteremka majiani mjini Washington na katika miji mengine kadhaa kote ulimwenguni kulalamika dhidi ya vita nchini Irak.Maandamano hayo yamefanyika siku chache tuu kabla ya kuadhimishwa miaka minne tangu vikosi vya Marekani na vile vya nchi shirika kuivamia Irak.Kwa mujibu wa polisi ya Marekani,waandamanaji 20 elfu waliandamana hadi wizara ya ulinzi wakidai wanajeshi wa Marekani wajereshwe nyumbani.Barani Ulaya,maandamano yameripotiwa mijini Madrid,Istanbul,Copenhagen,Prag,Athens na Nicosia.Maandamano makubwa yatakayofuatiwa na mhadhara yanatazamiwa kufanyika hii leo mjini New-York.Wakati huo huo waziri mkuu wa Australia John Howard,mshirika mkubwa wa rais George W. Bush wa Marekani,amekutana na waziri mkuu wa Irak Nouri el Maliki mjini Baghdad.Waziri mkuu Howard amemhakikishia kiongozi mwenzake ,vikosi vya Australia vitaendelea kuwepo Irak kwa wakati wote watakaohitajika.Na hayo yakiendeleya wanajeshi sita zaidi wa Marekani wameuwawa nchini Irak.Zaidi ya wanajeshi 3200 wa Marekani wameuwawa nchini Irak tangu vikosi vya nchi shirika vilipoivamia nchi hiyo March 20 mwaka 2003.