1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani

Josephat Nyiro Charo18 Juni 2010

Hali ya wakimbizi nchini Kenya bado ni mbaya. Shirika la UNHCR linasema Kenya inawapa hifadhi wakimbizi wapatao 964,000 wakiwemo laki moja unusu wa ndani

https://p.dw.com/p/NwwE
Wakimbizi wa kisomali wakicheza kwenye maji nje ya kambi ya wakimbizi ya Daadab, kaskazini mwa KenyaPicha: AP

Idadi ya wakimbizi nchini Kenya walio chini ya Shilika la Umoja wa mataifa la wakimbizi UNHCR inatarajiwa kuongezeka kutoka laki 660,000 mwaka huu hadi 681,000 ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao. Kwa mujibu wa takwimu kutoka shirika la UNHCR, Kenya inawapa hifadhi wakimbizi wapatao 964,000 wakiwemo laki moja unusu wa ndani maarufu IDPs. Idadi kubwa ya wakimbizi hao wanaishi katika kambi mbili za wakimbizi za Daadab kaskazini mashariki mwa Kenya na Kakuma huko Kaskazini huku wachache wakijitegemea wenyewe katika sehemu mbalimbali za nchi.

Mwandishi wetu Alfred Kiti Kutoka Nairobi ametuandalia taarifa hiyo wakati huu wa maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani.