1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

München yataka Transrapid

Oummilkheir26 Septemba 2007

Eti kweli treni hiyo ya mwemndo wa kasi itajengwa kama anavyotaka Stoiber

https://p.dw.com/p/CHRk

Mada tatu zimehanikiza magazetini hii leo:ujenzi wa njia ya treni za mwendo wa kasi-Transrapid nchini Ujerumani,mkutano wa baraza kuu la Umoja wa mataifa mjini New-York na mpango wa kupandishwa bei za safari za treni nchini Ujerumani.

Kwa mujibu wa gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG,licha ya matamshi ya waziri mkuu wa jimbo la Bavaria,Edmund Stoiber,bado hakuna makubaliano yaliyofikiwa kuhusu ujenzi wa njia ya treni ya mwendo wa kasi mjini München,isipokua tuu………..

“pamefikiwa makubaliano ya kiwango cha fedha kugharimia mradi huo ,kiwango ambacho, kila mmoja anakiri, ni cha chini kupita kiasi .Makubaliano halisi yatawezekana tuu ikiwa maandalizi ya mpango mzima yamekamilishwa na madai yaliyopelekwa mahakamani yameshindwa pia.Hakuna yeyote anaebisha kwamba ufundi wakuvutia na wa hali ya juu utatumika katika ujenzi wa njia hiyo.”haitakua nuru ya kiteknolojia lakini itakayong’ara mjini München.Jengine la kuvutia ni lile gurudumu kubwa kupita kiasi.Sera za kiimambo leo za usafiri,zinabidi ziwalenge zaidi binaadam na bidhaa pia ili waweze kutoka barabarani na kuingia badala yake katika treni.Kile ambacho serikali ya shirikisho na serikali za majimbo zitachanagia ili kuigharimia ujenzi wa njia ya treni ya mwendo wa kasi,kinakosekena katika shughuli za usafiri wa treni za masafa ya karibu, kimkoa na kitaifa-huko ndiko mafedha chungu nzima kama hayo yangeweza kuleta tija kubwa zaidi-linahisi gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG.

Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG linaandika:

„Kiu cha Stoiber kwa mradi wa Transrapid ni sawa na kiu alichokua nacho mshauri wake Strauss kwa mradi wa AIRBUS.Mradi wa teknolojia ya hali ya juu ambao,ukikamilika daima utafungamanishwa na jina lake.Suala linalozuka ni jee amechagua mradi unaofaa,ili aweze kuingia katika madaftari ya historia ya kiufundi japo yeye ni mwanasiasa?Mradi wa treni inayoambaa katika ujia wa smaku ulipata sifa mapema miaka ya 80,njia ya treni hiyo ilipojengwa Emsland.Wakati ule uamuzi wa serikali kuu wa kuzidisha njia za reli ungeweza kudurusika.Na pengine hata gharama zisingekua ghali hivyo.Lakini tangu njia za reli za kawaida kuzidishwa,mradi wa Transrapid unaning’inia.

„Kansela Angela Merkel na hotuba yake mbele ya baraza kuu la Umoja wa mataifa ni mada iliyochambuliwa na gazeti la DRESDNER NEUESTEN NACHRICHTEN:

„Shirikisho la jamhuri ya Ujerumani linachangia katika juhudi kadhaa za kulinda amani na linatioa misaada pia.Mwenye kuwajibika namna hiyo,anastahiki pia kupigania kua na sauti kule maamuzi yanakopitishwa.Sio kwa kiu cha kutaka ukubwa,bali kuambatana na juhudi za Ujerumani.Kwa hivyo ilikua vyema kumuona kansela Angela Merkel mjini New York, akizungumzia sio tuu suala la hali ya hewa,bali pia mageuzi ya taasisi za umoja wa mataifa.Na ni sawa pia aliponyanyua sauti kutanabahisha kwamba baraza la usalama namna lilivyo hivi sasa haliambatani na ukweli wa mambo.Ujerumani inastahiki kuwa mwanachama wa baraza hilo-majukumu yote inayabeba-linaandika gazeti la DRESDNER NEUESTEN NACHRICHTEN.

GENERAL ASNZEIGER la mjini Bonn linahisi kansela Angela Merkel ameweka wazi kabisa,suala hapa si kujipeleka mbele Ujerumani,bali kuiambatanisha jumuia ya kimataifa na hali mpya iliyochomoza.