1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lusaka. Wakimbizi waanza kurejeshwa.

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuA

Shirika la umoja wa mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR, limeanza kuwarejesha kundi la kwanza la Wakongo 60,000 kutoka Zambia chini ya mpango wa miaka mitatu wa kurejea kwa hiari.

Msemaji wa UNHCR Kelvin Shimo amesema wakimbizi 20,000 watarejeshwa kwanza nchini jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo , kwa msaada wa serikali ya Zambia katika mwaka huu 2007 na 40,000 wataanza kurejea nyumbani mwakani 2008.

Zambia inawahifadhi maelfu ya wakimbizi kutoka Kongo ambao walikimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 1998-2003 nchini mwao wakati makundi ya waasi yalipoanzisha mashambulizi dhidi ya mji mkuu Kinshasa katika jitihada za kuuangusha utawala wa rais wa zamani marehemu Laurent Kabila.