1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA: Rais wa zamani wa Zambia amelazwa hospitali

25 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByX

Rais wa zamani wa Zambia,Frederick Chiluba amelazwa hospitali baada ya kuzirai hiyo jana,ikiwa ni siku chache tu kabla ya kufanyiwa ukaguzi wa matibabu,kuona iwapo afya yake itamruhusu kukabiliana na kesi ya rushwa.Msemaji wake,Emmmanuel Mwamba amesema,Chiluba alianguka nyumbani kwake siku ya Alkhamisi.Chiluba,mwenye umri wa miaka 64 aliwahi kutibiwa kwa matatizo ya moyo,alipokuwa akichunguzwa kuhusika na kesi yake.Madaktari wa Zambia walitaka kuona iwapo Chiluba ni mzima wa kutosha kufika mahakamani.