1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA : Rais aonya upinzani kwa mashtaka ya uhaini

10 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Gv

Rais Levy Mwanawasa wa Zambia ameuonya upinzani na makundi ya kiraia kwamba watakabiliwa na mashtaka ya uhaini iwapo watapinga mipango ya serikali yake kurekebisha katiba.

Radio ya NBC imesema Rais Mwanawaswa amesema watu wanaothubutu kuikaidi serikali yake juu Mkutano wa Katiba ya Taifa watakamatwa kwa uhaini.

Hapo mwaka 2004 Zambia ilianzisha kamisheni ya marekebisho ya katiba ambayo ilizuru nchi nzima kukusanya maoni na kupendekeza kwamba katiba inapaswa kupitishwa na baraza la watu wenye busara kabla ya kuidhinishwa na bunge.