1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LRA yashutumiwa kuwadhalilisha watoto:UN

7 Juni 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki -moon, amewasilisha ripoti yake juu ya makosa ya kuwauwa na kuwadhalilisha watoto yanayofanywa na Joseph Kony, akiongoza kundi la waasi wa LRA, yakiwa ya kutisha.

https://p.dw.com/p/159z0
Katibu Mkuu wa UN
Katibu Mkuu wa UNPicha: dapd

Wakati huohuo,serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imekosolewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa vile vyombo vyake vya ulinzi na usalama vimekiuka kwa hali ya juusana haki za binadamu.Kwa kipindi cha miongo mitatu akiwa msituni, Joseph Kony, kiongozi wa kundi la waasi hao, anahusishwa na mauaji ya makumi elfu ya watu, ambapo watoto wanatumika kama watumwa wa ngono.

Joseph Kony
Joseph KonyPicha: AP

LRA yaua watoto mamia

Ripoti hiyo iliyotolewa imebainisha kuwa kati ya Julai 2009 na Februari 2012 kikundi hicho kimewaua watoto 591, ambapo wasichana ni 268 na wavulana 323 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya kati tu.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa watoto hao wanatumika katika shughuli mbalimbali kama vile kupika, wapagazi wa mizigo, walinzi, wapelelezi na kufanya shughuli zingine. Kukiwa na watoto kadhaa waliowahi kuwatumikia waasi hao, inatajwa kuwa wanatumika katika kuwauwa watoto wenzao au kutumika katika vitendo vya ngono mara kadhaa, pia wanashurutishwa kuolewa na makamanda na askari wengine katika kikosi hicho bila ya wao wenyewe kukubali.

Shuhuda wa mateso ya Kony wanasimulia

Grace Akallo, ambaye ni miongoni mwao, aliingizwa katika kundi la waasi la NRA mwaka1996, ambapo miezi saba baadae alifanikiwa kutoroka. Yeye anasema wazi kuwa alipokuwa huko alipata mafunzo ya kina ya kutumia silaha kubwa kubwa, kama vile AK 47, na aliona rafiki zake wakishurutishwa kuwaua wazazi wao bila ya woga wowote ule.

Lakini kwa sasa mataifa kadhaa yanajipanga kuongeza nguvu ya pamoja kuanza kumsaka Joseph Konyi, ambaye anaendesha vita hivyo vya msituni, ili kuweza kumfikisha katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa binadamu. Mataifa hayo ni Sudan Kusini, Kongo na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Jamhuri ya Afrika ya Kati yanyooshewa kidole

Watoto
WatotoPicha: DW

Wakati huo huo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeilaumu serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa vyombo vyake vya usalama kutokujali haki za binadamu na kuitaka nchi hiyo ianzishe uchunguzi mara moja.

Magrgaret Vogt, Mjumbe wa Umoja wa Mataifa, amesema katika ufunguzi wa Baraza hilo kuwa vyombo vya usalama vya taifa hilo, kikiwamo kikosi maalumu cha ulinzi wa rais, vinajiingiza katika kukiuka haki za binadamu kama vile kuwaweka kizuizini baadhi ya watu. Kun a pia udahalilishajii wa kila aina unafanywa bila ya kufikishwa wanaohusika kufikishwa mahakamani. Taifa hilo lina watu 75,000 ambao wanaishi katika hali ya mashaka, huku kukiweko dola milioni 134 zilitolewa msaada kwa watu hao hazijulikana zilivyotumika.

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kwa pamoja limeziomba Chad, Jamhuri ya Afrika ya kati na Sudan kusaidia kufanikisha kukakmatwa kwa Joseph Konyi na kikundi chake cha LRA, huku kukitolewa ahadi ya kutolewa ushirikiano mkubwa kutoka Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.

Mwandishi:Adeladius Makwega/DPAE/AFPERTRE

Mhariri: Miraji Othman