1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Washukiwa wengine wawili wakamatwa

2 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmS

Polisi nchini Uingereza wamewakamata washukiwa wengine wawili wanaoaminika kuhusika na majaribio ya mashambulio ya mabomu mwishoni mwa juma lililopita katika miji ya London na Glasgow.

Kwa mujibu wa polisi washukiwa watano wamekamatwa mpaka sasa.Hakuna aliyejeruhiwa katika majaribio hayo mawili ya mashambulio.Uingereza inachukua tahadhari zote ili kukabiliana na ugaidi huku ilani zikitolewa kote nchini.

Gordon Brown ni Waziri Mkuu wa Uingereza na alisema kuwa.

''Tunalazimika kuwa chonjo wakati wote na kuchukua tahadhari zote.Nadhani ujumbe tunaotoa ni kwamba raia wote wa Uingereza kwa pamoja hatutakubali,hatutatishika na hatutaruhusu maisha yetu kuathiriwa.''

Siku ya jumamosi watu wawili waliegesha lori dogo katika eneo la kuwalaki abiria kwenye Uwanja wa ndege wa Glasgow.Mmoja wa washukiwa waliohusika ndiye aliyejeruhiwa pekee katika shambulio hilo ambaye kwa sasa bado yuko hospitali baada ya kuchomeka vibaya sana.

Wakati huohuo chama cha wafanyikazi kinachowakilisha polisi nchini hapa Ujerumani kinaonya kuwa mashambulio kama hayo ya Uingereza huenda yakatokea. Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schaüble anatoa wito wa kuongezwa idadi ya kamera maalum za uangalizi katika viwanja vya ndege na maeneo mengine ya usafiri mkubwa.Hata hivyo baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani wanashtumu wazo hilo.