LONDON.Washukiwa wawili waachiliwa huru | Habari za Ulimwengu | DW | 07.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON.Washukiwa wawili waachiliwa huru

Washukiwa wawili wameachiliwa huru kati ya washukiwa tisa waliokamatwa mjini London nchini Uingereza wiki iliyopita kwa tuhuma za kupanga njama za kumteka nyara na kumkata kichwa mwanajeshi mmoja muislamu wa jeshi la Uingereza.

Washukiwa hao waliachiliwa huru baada ya mahakama kukataa ombi la upande wa mashtaka lililotaka waendelee kuzuiliwa zaidi.

Wakili wa watuhumiwa hao alidai mahakamani kwamba upande wa mashtaka ulishindwa kueleza sababu ya kukamatwa kwa wateja wake.

Vilevile mahakama hiyo imeipa polisi ya London muda wa saa 72 kukamilisha mahojiano na washukiwa saba waliosalia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com