1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:waharibifu wa watoto wakamatwa !

19 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqS

Polisi ya Uingereza imefanikiwa kuvunja mtandao wa kimataifa wa waharibifu wa watoto.

Katika zoezi hilo Polisi hao waliwaokoa watoto 31 na kuwakamata watuhumiwa 700 katika sehemu mbalimbali za dunia.

Wapelelezi wa Uingereza walikipelemba chumba cha internet ambapo watuhumiwa walikuwa wanabadilishana maalfu ya picha na filamu za watoto zinazoonesha mitindo ya ngono.