1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Uingereza yasema Iran itakabiliwa na vikwazo zaidi isipokomesha mradi wake

3 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5G

Uingereza imesema ikiwa Iran itashindwa kukomesha mradi wake wa kurutubisha madini ya Uranium itakabiliana na vikwazo vingine vya Umoja wa Mataifa.

Matamshi hayo yametolewa baada ya kufanyika mkutano wa maafisa wa nchi tano za kudumu kwenye baraza la usalama la Umoja wa mataifa,Uingereza China Ufaransa,Urussi na Marekani pamoja na Ujerumani. Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imefahamisha katika taarifa yake kwamba nchi zote sita zimekubaliana kuhusu hatua ya baadae ya kuchukuliwa.

Nchi hizo pia zimesema zinamuunga mkono mkuu wa sera za umoja wa ulaya Javier Solana katika kuendelea na mazungumzo na Iran.Iran imesisitiza kwamba itaendelea na mpango wake wa Kinuklia.