1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Uingereza na Iran zalainisha misimamo yao

3 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCq

Iran na Uingereza huenda zikalainisha misimamo yao katika suluhisho la kadhia ya kukamatwa kwa wanamaji 15 wa Uingereza, huko Iran.

Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Iran, Ali Larajani akizungumza na televisheni ya Uingereza amesema kuwa wanamaji hao huenda wakaachiwa huru bila ya kushtakiwa.

Uingereza kwa upande wake imesema kuwa kauli hiyo ya Larajani ni dalili ya suala hilo kumalizika kwa njia za kidiplomasia.

Wakati huo huo mkutano uliyokuwa ufanyike leo kati ya waandishi wa habari na Rais Mahamoud Ahmednejad umeahirishwa hadi kesho.

Hayo yakiendelea, Marekani imesema kuwa inataka maelezo kujua wapi alipo raia wake mmoja ambaye inaarifiwa amepotea huko kusini mwa Iran.