1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Nchi zenye nguvu kujadili juu ya kupitisha vikwazo vikali dhidi ya Iran

31 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BC

Mataifa yenye nguvu duniani yanapanga kukutana nchini Uingereza wiki hii pamoja na shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi ya technologia ya Nuklia IAEA kujadili vikwazo vipya dhidi ya Iran juu ya mpango wake wa kinuklia.

Maafisa kutoka nchi tano wanachama wa kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani watakutana mwishoni mwa wiki hii mjini London.Mkutano huo ulitakiwa kufanyika wiki mbili zilizopita lakini China ilijiondoa.Mkutano huo unalenga kujadili uwezekano wa duru ya tatu ya azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa la kuiwekea vikwazo vikali zaidi Iran kwa kukaidi amri ya kuitaka isimamishe mpango wake wa Kinuklia.Mataifa hayo yalikubaliana mwishoni mwa mwezi Septemba kuchelewesha kura juu ya kupitisha vikwazo hivyo dhidi ya Iran kwa lengo la kusubiri ripoti zitakazotolewa Novemba na shirika la IAEA na mpatanishi wa Umoja wa Ulaya katika suala la Iran.