1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Marekani yaonywa dhidi ya kuishambulia Iran

5 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUz

Watu wenye hekima nchini Uingereza wameionya Marekani dhidi ya kuishambulia Iran.

Watu hao wamesema kuwa shambulio lolote dhidi ya Iran litasababisha maafa makubwa katika mashariki ya kati na sehemu zingine.Watu hao wametahadharisha juu ya maafa hayo katika ripoti iliyotolewa leo mjini London.

Ripoti hiyo imetolewa kufuatia uvumi kwamba Marekani inajiandaa kuishambulia Iran kijeshi.

Marekani pia imeambiwa kuwa kuishambulia Iran,kutaiyumbisha zaidi Irak na kutaondoa matumaini ya kuleta amani baina ya Israel na Palestina na vile vile kutasababisha bei ya mafuta kupanda na kuathiri uchumi wa dunia nzima.

Ripoti hiyo imetayarishwa na makundi 17 ikiwa pamoja na ya vyama vya wafanyakazi na jumuiya za kidini nchini Uingereza.