LONDON:Maadhimisho ya siku ya Darfur duniani | Habari za Ulimwengu | DW | 09.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON:Maadhimisho ya siku ya Darfur duniani

Leo ni siku ya maadhimisho ya jimbo la Darfur duniani.

Kundi la wanawake mashuhuri limesema jumuiya ya kimataifa lazima ipeleke wanajeshi wa kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan kuwalinda wanawake dhidi ya ubakaji.

Akiwemo waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Madeline Albright na mwanaharakati wa haki za watoto Graca Michel kundi hilo limesema ubakaji na unyanyasaji wa wanawake ni mambo yanayofanyika kila siku kama silaha ya vita katika jimbo la Darfur.

Viongozi hao wamesikitishwa na jinsi wanawake na wasichana wanavyoishi katika hofu ya kushambuliwa wakati serikali ya Sudan ikionyesha kutokuwa tayari kuwalinda raia wake.

Maadhimisho ya siku hii yanafanyika katika nchi 40 kwa ajili ya jimbo la Darfur ambako zaidi ya watu 200,000 wameuwawa na wengine milioni 2 na nusu wameachwa bila makaazi tangu kuzuka kwa mapigano kati ya waasi na serikali mwaka 2003.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com